Luka Mlango 7 Luke

Luka 7:1 Luke 7:1

Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.

Luka 7:2 Luke 7:2

Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.

Luka 7:3 Luke 7:3

Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.

Luka 7:4 Luke 7:4

Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili;

Luka 7:5 Luke 7:5

maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.

Luka 7:6 Luke 7:6

Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu;

Luka 7:7 Luke 7:7

kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.

Luka 7:8 Luke 7:8

Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

Luka 7:9 Luke 7:9

Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.

Luka 7:10 Luke 7:10

Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.

Luka 7:11 Luke 7:11

Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa.

Luka 7:12 Luke 7:12

Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.

Luka 7:13 Luke 7:13

Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie.

Luka 7:14 Luke 7:14

Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.

Luka 7:15 Luke 7:15

Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.

Luka 7:16 Luke 7:16

Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake.

Luka 7:17 Luke 7:17

Habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote, na katika nchi zote za kando kando.

Luka 7:18 Luke 7:18

Wanafunzi wa Yohana wakamletea habari za hayo yote.

Luka 7:19 Luke 7:19

Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

Luka 7:20 Luke 7:20

Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

Luka 7:21 Luke 7:21

Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.

Luka 7:22 Luke 7:22

Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.

Luka 7:23 Luke 7:23

Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.

Luka 7:24 Luke 7:24

Basi, wajumbe wa Yohana walipokwisha ondoka, alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?

Luka 7:25 Luke 7:25

Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokula raha, wamo katika majumba ya kifalme.

Luka 7:26 Luke 7:26

Lakini, mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na aliye zaidi ya nabii.

Luka 7:27 Luke 7:27

Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.

Luka 7:28 Luke 7:28

Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana; lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.

Luka 7:29 Luke 7:29

Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.

Luka 7:30 Luke 7:30

Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye.

Luka 7:31 Luke 7:31

Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini?

Luka 7:32 Luke 7:32

Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.

Luka 7:33 Luke 7:33

Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo.

Luka 7:34 Luke 7:34

Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.

Luka 7:35 Luke 7:35

Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.

Luka 7:36 Luke 7:36

Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.

Luka 7:37 Luke 7:37

Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.

Luka 7:38 Luke 7:38

Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.

Luka 7:39 Luke 7:39

Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.

Luka 7:40 Luke 7:40

Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena.

Luka 7:41 Luke 7:41

Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini.

Luka 7:42 Luke 7:42

Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi?

Luka 7:43 Luke 7:43

Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki.

Luka 7:44 Luke 7:44

Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.

Luka 7:45 Luke 7:45

Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu.

Luka 7:46 Luke 7:46

Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.

Luka 7:47 Luke 7:47

Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.

Luka 7:48 Luke 7:48

Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.

Luka 7:49 Luke 7:49

Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi?

Luka 7:50 Luke 7:50

Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani.