Yeremia Mlango 22 Jeremiah

Yeremia 22:1 Jeremiah 22:1

Bwana akasema hivi, Shuka nyumbani kwa mfalme wa Yuda, ukaseme neno hili huko,

Yeremia 22:2 Jeremiah 22:2

ya kwamba, Sikia neno la Bwana, Ee mfalme wa Yuda; wewe uketiye katika kiti cha enzi cha Daudi, wewe, na watumishi wako, na watu wako wote waingiao kwa malango haya;

Yeremia 22:3 Jeremiah 22:3

Bwana asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.

Yeremia 22:4 Jeremiah 22:4

Kwa maana mkifanya haya kweli kweli, ndipo watakapoingia kwa malango ya nyumba hii wafalme wenye kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi, wanakwenda kwa magari, na wamepanda farasi yeye, na watumishi wake, na watu wake.

Yeremia 22:5 Jeremiah 22:5

Lakini kama hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa.

Yeremia 22:6 Jeremiah 22:6

Kwa maana Bwana asema hivi, katika habari ya nyumba ya mfalme wa Yuda; Wewe u Gileadi kwangu, na kichwa cha Lebanoni; Ila hakika nitakufanya kuwa jangwa, na miji isiyokaliwa na watu.

Yeremia 22:7 Jeremiah 22:7

Nami nitakufanyia tayari watu wenye kuharibu, kila mtu na silaha zake; Nao watakata mierezi miteule yako, na kuitupa motoni.

Yeremia 22:8 Jeremiah 22:8

Na mataifa mengi watapita karibu na mji huu, nao watasema kila mtu na jirani yake, Nini maana yake Bwana kuutenda hivi mji huu mkubwa?

Yeremia 22:9 Jeremiah 22:9

Ndipo watakapojibu, Ni kwa sababu waliliacha agano la Bwana, Mungu wao, wakaabudu miungu mingine, na kuitumikia.

Yeremia 22:10 Jeremiah 22:10

Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee, Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali; Kwa maana yeye hatarudi tena, Wala hataiona nchi aliyozaliwa.

Yeremia 22:11 Jeremiah 22:11

Maana Bwana asema hivi, katika habari za Shalumu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; aliyemiliki badala ya Yosia, baba yake, yeye aliyetoka mahali hapa; Hatarudi huku tena;

Yeremia 22:12 Jeremiah 22:12

bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe.

Yeremia 22:13 Jeremiah 22:13

Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;

Yeremia 22:14 Jeremiah 22:14

Asemaye, Nitajijengea nyumba pana na vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.

Yeremia 22:15 Jeremiah 22:15

Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa.

Yeremia 22:16 Jeremiah 22:16

Alihukumu maneno ya maskini na mhitaji; hapo ndipo alipofanikiwa. Je! Huku siko kunijua, asema Bwana?

Yeremia 22:17 Jeremiah 22:17

Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.

Yeremia 22:18 Jeremiah 22:18

Basi, Bwana asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.

Yeremia 22:19 Jeremiah 22:19

Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.

Yeremia 22:20 Jeremiah 22:20

Haya panda Lebanoni, ukalie Upalize sauti yako katika Bashani; Ukalie kutoka Abarimu; Maana wapenzi wako wote wameangamia.

Yeremia 22:21 Jeremiah 22:21

Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.

Yeremia 22:22 Jeremiah 22:22

Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.

Yeremia 22:23 Jeremiah 22:23

Wewe ukaaye Lebanoni, Ufanyaye kioto chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo utungu kama wa mwanamke azaaye.

Yeremia 22:24 Jeremiah 22:24

Kama niishivyo mimi, asema Bwana, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung'oa wewe hapo;

Yeremia 22:25 Jeremiah 22:25

nami nitakutia katika mikono ya watu wale wakutafutao roho yako, na katika mikono yao unaowaogopa, naam, katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya Wakaldayo.

Yeremia 22:26 Jeremiah 22:26

Nami nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende nchi nyingine ambayo hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko.

Yeremia 22:27 Jeremiah 22:27

Lakini nchi ile ambayo wanatamani kuirudia, hawatairudia kamwe.

Yeremia 22:28 Jeremiah 22:28

Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua?

Yeremia 22:29 Jeremiah 22:29

Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.

Yeremia 22:30 Jeremiah 22:30

Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.