Yeremia Mlango 15 Jeremiah

Yeremia 15:1 Jeremiah 15:1

Ndipo Bwana akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.

Yeremia 15:2 Jeremiah 15:2

Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, Bwana asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.

Yeremia 15:3 Jeremiah 15:3

Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema Bwana; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.

Yeremia 15:4 Jeremiah 15:4

Nami nitawafanya kuwa kitu cha kutisha katika falme zote za duniani, kwa sababu ya Manase, mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa sababu ya mambo aliyoyatenda katika Yerusalemu.

Yeremia 15:5 Jeremiah 15:5

Maana ni nani atakayekuhurumia, Ee Yerusalemu? Au ni nani atakayekulilia? Au ni nani atakayegeuka upande ili kuuliza habari za hali yako?

Yeremia 15:6 Jeremiah 15:6

Umenikataa mimi, asema Bwana, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi.

Yeremia 15:7 Jeremiah 15:7

Nami nimewapepea kwa kipepeo katika malango ya nchi nimewaondolea watoto wao, nimewaharibu watu wangu; hata hivyo hawakurudi na kuziacha njia zao.

Yeremia 15:8 Jeremiah 15:8

Wajane wao wameongezeka kwangu kuliko mchanga wa bahari; nimeleta mwenye kuteka wakati wa adhuhuri juu ya mama wa vijana; nimeleta hamu na maogofyo yampate ghafula.

Yeremia 15:9 Jeremiah 15:9

Mwanamke aliyezaa watoto saba anazimia; ametoa roho; jua lake limekuchwa, ungali ni wakati wa mchana; ametahayarika na kufedheheka; na mabaki yao nitawatoa kwa upanga mbele ya adui zao, asema Bwana.

Yeremia 15:10 Jeremiah 15:10

Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.

Yeremia 15:11 Jeremiah 15:11

Bwana akasema, Hakika nitakutia nguvu upate mema; hakika nitamlazimisha adui akusihi wakati wa uovu, na wakati wa taabu.

Yeremia 15:12 Jeremiah 15:12

Je! Mtu aweza kuvunja chuma, naam, chuma kitokacho kaskazini, au shaba?

Yeremia 15:13 Jeremiah 15:13

Mali yako na hazina zako nitazitoa kuwa nyara, bila kulipwa thamani yake; naam, kwa sababu ya dhambi zako zote, hata katika mipaka yako yote.

Yeremia 15:14 Jeremiah 15:14

Nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana moto umewashwa katika hasira yangu, utakaowateketeza ninyi.

Yeremia 15:15 Jeremiah 15:15

Ee Bwana, unajua wewe; unikumbuke, unijilie, ukanilipie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na mashutumu.

Yeremia 15:16 Jeremiah 15:16

Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.

Yeremia 15:17 Jeremiah 15:17

Sikuketi katika mkutano wao wanaojifurahisha, wala sikufurahi, naliketi peke yangu kwa sababu ya mkono wako; kwa maana umenijaza ghadhabu.

Yeremia 15:18 Jeremiah 15:18

Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha yangu haina dawa, inakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?

Yeremia 15:19 Jeremiah 15:19

Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.

Yeremia 15:20 Jeremiah 15:20

Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana.

Yeremia 15:21 Jeremiah 15:21

Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.