Yeremia Mlango 23 Jeremiah

Yeremia 23:1 Jeremiah 23:1

Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema Bwana.

Yeremia 23:2 Jeremiah 23:2

Kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema Bwana.

Yeremia 23:3 Jeremiah 23:3

Nami nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.

Yeremia 23:4 Jeremiah 23:4

Nami nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema Bwana.

Yeremia 23:5 Jeremiah 23:5

Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.

Yeremia 23:6 Jeremiah 23:6

Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.

Yeremia 23:7 Jeremiah 23:7

Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri;

Yeremia 23:8 Jeremiah 23:8

lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.

Yeremia 23:9 Jeremiah 23:9

Katika habari za manabii. Moyo wangu ndani yangu umevunjika, Mifupa yangu yote inatikisika. Nimekuwa kama mtu aliye mlevi, Na kama mtu aliyeshindwa na divai;kwa ajili ya Bwana,na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.

Yeremia 23:10 Jeremiah 23:10

Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.

Yeremia 23:11 Jeremiah 23:11

Maana nabii, na kuhani, wote wawili wanakufuru; naam, katika nyumba yangu nimeuona uovu wao, asema Bwana.

Yeremia 23:12 Jeremiah 23:12

Kwa ajili ya hayo njia yao itakuwa kwao kama mahali pa kuteleza gizani; watatelemshwa na kuanguka hapo; kwa maana nitaleta uovu juu yao, naam, mwaka wa kujiliwa kwao, asema Bwana.

Yeremia 23:13 Jeremiah 23:13

Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli.

Yeremia 23:14 Jeremiah 23:14

Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.

Yeremia 23:15 Jeremiah 23:15

Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.

Yeremia 23:16 Jeremiah 23:16

Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha Bwana.

Yeremia 23:17 Jeremiah 23:17

Daima huwaambia wao wanaonidharau, Bwana amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote.

Yeremia 23:18 Jeremiah 23:18

Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la Bwana, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?

Yeremia 23:19 Jeremiah 23:19

Tazama, tufani ya Bwana, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni dhoruba ya kisulisuli; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.

Yeremia 23:20 Jeremiah 23:20

Hasira ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa.

Yeremia 23:21 Jeremiah 23:21

Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri.

Yeremia 23:22 Jeremiah 23:22

Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao.

Yeremia 23:23 Jeremiah 23:23

Mimi ni Mungu aliye karibu, asema Bwana, mimi si Mungu aliye mbali.

Yeremia 23:24 Jeremiah 23:24

Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana.

Yeremia 23:25 Jeremiah 23:25

Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto.

Yeremia 23:26 Jeremiah 23:26

Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe?

Yeremia 23:27 Jeremiah 23:27

Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali.

Yeremia 23:28 Jeremiah 23:28

Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana.

Yeremia 23:29 Jeremiah 23:29

Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?

Yeremia 23:30 Jeremiah 23:30

Basi kwa sababu hiyo mimi ni juu ya manabii hao, asema Bwana, wanaompokonya kila mtu jirani yake maneno yangu.

Yeremia 23:31 Jeremiah 23:31

Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema Bwana, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema,

Yeremia 23:32 Jeremiah 23:32

Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema Bwana, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema Bwana.

Yeremia 23:33 Jeremiah 23:33

Na watu hawa, au nabii au kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa Bwana ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo gani? Bwana asema, Nitawatupilia mbali.

Yeremia 23:34 Jeremiah 23:34

Na katika habari ya nabii, na kuhani, na watu, watakaosema, Mzigo wa Bwana, mimi nitamwadhibu mtu yule, na nyumba yake.

Yeremia 23:35 Jeremiah 23:35

Mtasema hivi kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, Bwana amejibu mtu? Na, Bwana amesemaje?

Yeremia 23:36 Jeremiah 23:36

Na mzigo wa Bwana hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya Bwana wa majeshi, Mungu wetu.

Yeremia 23:37 Jeremiah 23:37

Nawe utamwambia nabii hivi, Bwana amekujibu nini? Na, Bwana amesemaje?

Yeremia 23:38 Jeremiah 23:38

Lakini mkisema, Mzigo wa Bwana, basi, Bwana asema hivi, Kwa sababu mwasema neno hili, ; nami nimemtuma mtu kwenu kusema, Msiseme, ;

Yeremia 23:39 Jeremiah 23:39

basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu;

Yeremia 23:40 Jeremiah 23:40

nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.