Yeremia Mlango 30 Jeremiah

Yeremia 30:1 Jeremiah 30:1

Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,

Yeremia 30:2 Jeremiah 30:2

Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.

Yeremia 30:3 Jeremiah 30:3

Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.

Yeremia 30:4 Jeremiah 30:4

Na haya ndiyo maneno aliyosema Bwana, katika habari za Israeli, na katika habari za Yuda.

Yeremia 30:5 Jeremiah 30:5

Maana Bwana asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.

Yeremia 30:6 Jeremiah 30:6

Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona utungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi.

Yeremia 30:7 Jeremiah 30:7

Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.

Yeremia 30:8 Jeremiah 30:8

Na itakuwa katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, nitaivunja nira yake itoke shingoni mwako, nami nitavipasua vifungo vyako; wala wageni hawatamtumikisha tena;

Yeremia 30:9 Jeremiah 30:9

bali watamtumikia Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao.

Yeremia 30:10 Jeremiah 30:10

Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema Bwana; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.

Yeremia 30:11 Jeremiah 30:11

Maana mimi ni pamoja nawe, asema Bwana, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.

Yeremia 30:12 Jeremiah 30:12

Maana Bwana asema hivi, Maumivu yako hayaponyekani, na jeraha yako ni kubwa.

Yeremia 30:13 Jeremiah 30:13

Hapana mtu wa kukutetea; kwa jeraha yako huna dawa ziponyazo.

Yeremia 30:14 Jeremiah 30:14

Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha ya adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.

Yeremia 30:15 Jeremiah 30:15

Mbona unalilia maumivu yako? Hayaponyeki maumivu yako; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya.

Yeremia 30:16 Jeremiah 30:16

Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo.

Yeremia 30:17 Jeremiah 30:17

Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.

Yeremia 30:18 Jeremiah 30:18

Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.

Yeremia 30:19 Jeremiah 30:19

Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.

Yeremia 30:20 Jeremiah 30:20

Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wawaoneao.

Yeremia 30:21 Jeremiah 30:21

Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema Bwana.

Yeremia 30:22 Jeremiah 30:22

Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.

Yeremia 30:23 Jeremiah 30:23

Tazama, tufani ya Bwana, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani.

Yeremia 30:24 Jeremiah 30:24

Hasira kali ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kutenda, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtayafahamu haya.