Yeremia Mlango 10 Jeremiah

Yeremia 10:1 Jeremiah 10:1

Enyi nyumba ya Israeli, lisikieni neno awaambialo Bwana;

Yeremia 10:2 Jeremiah 10:2

Bwana asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo.

Yeremia 10:3 Jeremiah 10:3

Maana desturi za watu hao ni ubatili, maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi na shoka.

Yeremia 10:4 Jeremiah 10:4

Huupamba kwa fedha na dhahabu; huukaza kwa misumari na nyundo, usitikisike.

Yeremia 10:5 Jeremiah 10:5

Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.

Yeremia 10:6 Jeremiah 10:6

Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee Bwana; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.

Yeremia 10:7 Jeremiah 10:7

Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa yako wewe; kwa kuwa miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika hali yao ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama wewe.

Yeremia 10:8 Jeremiah 10:8

Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.

Yeremia 10:9 Jeremiah 10:9

Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawi na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi yao.

Yeremia 10:10 Jeremiah 10:10

Bali Bwana ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.

Yeremia 10:11 Jeremiah 10:11

Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu.

Yeremia 10:12 Jeremiah 10:12

Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.

Yeremia 10:13 Jeremiah 10:13

Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.

Yeremia 10:14 Jeremiah 10:14

Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.

Yeremia 10:15 Jeremiah 10:15

Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu; Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.

Yeremia 10:16 Jeremiah 10:16

Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila ya urithi wake; Bwana wa majeshi ndilo jina lake.

Yeremia 10:17 Jeremiah 10:17

Haya! Kusanya bidhaa yako katika nchi, wewe ukaaye katika mazingiwa.

Yeremia 10:18 Jeremiah 10:18

Maana Bwana asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.

Yeremia 10:19 Jeremiah 10:19

Ole wangu, kwa sababu ya jeraha yangu! Pigo langu laumia; lakini nalisema, Kweli, ni huzuni yangu mimi, nami sina budi kuivumilia.

Yeremia 10:20 Jeremiah 10:20

Hema yangu umetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hapana mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.

Yeremia 10:21 Jeremiah 10:21

Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa Bwana; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.

Yeremia 10:22 Jeremiah 10:22

Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.

Yeremia 10:23 Jeremiah 10:23

Ee Bwana, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.

Yeremia 10:24 Jeremiah 10:24

Ee Bwana, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza.

Yeremia 10:25 Jeremiah 10:25

Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.