Yeremia Mlango 48 Jeremiah

Yeremia 48:1 Jeremiah 48:1

Habari za Moabu. Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.

Yeremia 48:2 Jeremiah 48:2

Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njoni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.

Yeremia 48:3 Jeremiah 48:3

Sauti ya kilio toka Horonaimu, Ya kutekwa na uharibifu mkuu.

Yeremia 48:4 Jeremiah 48:4

Moabu umeharibika; Wadogo wake wamewasikiza watu kilio.

Yeremia 48:5 Jeremiah 48:5

Kwa maana watu wapandapo huko Luhithi Watapanda wasiache kulia; Nao watu watelemkapo huko Horonaimu Wameisikia huzuni ya kilio cha uharibifu.

Yeremia 48:6 Jeremiah 48:6

Haya! Kimbieni! Jiokoeni nafsi zenu! Mkawe kama mtu aliye mkiwa.

Yeremia 48:7 Jeremiah 48:7

Maana, kwa kuwa umeyatumainia matendo yako, na hazina zako, wewe nawe utatwaliwa; na Kemoshi atatoka aende katika uhamisho, makuhani wake na wakuu wake pamoja.

Yeremia 48:8 Jeremiah 48:8

Naye mwenye kuteka nyara atakuja juu ya kila mji, wala hapana mji utakaookoka; bonde nalo litaangamia, nayo nchi tambarare itaharibiwa; kama Bwana alivyosema.

Yeremia 48:9 Jeremiah 48:9

Mpe Moabu mabawa, apate kuruka na kwenda zake; na miji yake itakuwa ukiwa, isiwe na mtu wa kukaa ndani yake.

Yeremia 48:10 Jeremiah 48:10

Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.

Yeremia 48:11 Jeremiah 48:11

Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.

Yeremia 48:12 Jeremiah 48:12

Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.

Yeremia 48:13 Jeremiah 48:13

Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, matumaini yao.

Yeremia 48:14 Jeremiah 48:14

Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.

Yeremia 48:15 Jeremiah 48:15

Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wametelemka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana wa majeshi.

Yeremia 48:16 Jeremiah 48:16

Msiba wa Moabu umefika karibu, Na mateso yake yanafanya haraka.

Yeremia 48:17 Jeremiah 48:17

Ninyi nyote mnaomzunguka, mlilieni, Nanyi nyote mlijuao jina lake, semeni, Jinsi ilivyovunjika fimbo ya enzi, Fimbo ile iliyokuwa nzuri!

Yeremia 48:18 Jeremiah 48:18

Ee binti ukaaye Diboni, Shuka toka utukufu wako, ukae katika kiu; Maana atekaye Moabu amepanda juu yako, Ameziharibu ngome zako.

Yeremia 48:19 Jeremiah 48:19

Wewe ukaaye Aroeri, Simama kando ya njia upeleleze; Mwulize mwanamume akimbiaye na mwanamke atorokaye, Sema, Imetendeka nini?

Yeremia 48:20 Jeremiah 48:20

Moabu ameaibishwa, kwa maana amevunjika; Pigeni yowe na kulia; Tangazeni habari hii katika Arnoni, Ya kuwa Moabu ameharibika.

Yeremia 48:21 Jeremiah 48:21

Na hukumu imeifikilia nchi tambarare; juu ya Holoni, na juu ya Yasa, na juu ya Mefaathi;

Yeremia 48:22 Jeremiah 48:22

na juu ya Diboni, na juu ya Nebo, na juu ya Beth-diblathaimu;

Yeremia 48:23 Jeremiah 48:23

na juu ya Kiriathaimu, na juu ya Beth-gamuli, na juu ya Beth-meoni;

Yeremia 48:24 Jeremiah 48:24

na juu ya Keriothi, na juu ya Bozra, na juu ya miji yote ya nchi ya Moabu, iliyo mbali na iliyo karibu.

Yeremia 48:25 Jeremiah 48:25

Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema Bwana. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya Bwana

Yeremia 48:26 Jeremiah 48:26

na Moabu atagaa-gaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?

Yeremia 48:27 Jeremiah 48:27

Alionekana kati ya wevi? Maana kila umtajapo watikisa kichwa chako.

Yeremia 48:28 Jeremiah 48:28

Enyi mkaao Moabu, iacheni miji, Enendeni kukaa majabalini; Mkawe kama njiwa afanyaye kioto chake Katika ubavu wa mdomo wa shimo.

Yeremia 48:29 Jeremiah 48:29

Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyotakabari moyoni mwake.

Yeremia 48:30 Jeremiah 48:30

Najua ghadhabu yake, asema Bwana, ya kuwa si kitu; majisifu yake hayakutenda neno lo lote.

Yeremia 48:31 Jeremiah 48:31

Kwa sababu hiyo nitampigia yowe Moabu, naam, nitapiga kelele kwa ajili ya Moabu yote; nitawaombolezea watu wa Kir-heresi.

Yeremia 48:32 Jeremiah 48:32

Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hata bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.

Yeremia 48:33 Jeremiah 48:33

Furaha na shangwe zimeondoshwa, katika shamba lizaalo sana, na katika nchi ya Moabu; nami nimeikomesha divai katika mashinikizo; hapana mtu atakayekanyaga zabibu kwa shangwe; shangwe ile itakuwa si shangwe.

Yeremia 48:34 Jeremiah 48:34

Toka kilio cha Heshboni mpaka Eleale, naam, mpaka Yahasa, wametoa sauti zao, toka Soari mpaka Horonaimu, hata Eglath-shelishia; maana maji ya Nimrimu nayo yatakuwa ukiwa.

Yeremia 48:35 Jeremiah 48:35

Pamoja na hayo, asema Bwana, nitamkomesha katika Moabu mtu atoaye sadaka katika mahali pa juu, naye awafukiziaye uvumba miungu yake.

Yeremia 48:36 Jeremiah 48:36

Kwa sababu hiyo moyo wangu watoa sauti kama filimbi kwa ajili ya Moabu, na kwa ajili ya watu wa Kir-heresi, moyo wangu watoa sauti kama filimbi; kwa kuwa wingi aliojipatia umepotea.

Yeremia 48:37 Jeremiah 48:37

Maana kila kichwa kina upaa, na ndevu zote zimenyolewa; mikono yote ina alama za chale, na viuno vyote vimevikwa nguo za magunia.

Yeremia 48:38 Jeremiah 48:38

Juu ya dari zote za nyumba za Moabu, na katika njia kuu zake, pana maombolezo, kila mahali; kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema Bwana.

Yeremia 48:39 Jeremiah 48:39

Jinsi alivyovunjika! Pigeni yowe! Jinsi Moabu alivyogeuza kisogo kwa haya! Hivyo ndivyo Moabu atakavyokuwa dhihaka, na sababu ya kuwashangaza watu wote wamzungukao.

Yeremia 48:40 Jeremiah 48:40

Maana Bwana asema hivi, Tazama, ataruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Moabu.

Yeremia 48:41 Jeremiah 48:41

Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake.

Yeremia 48:42 Jeremiah 48:42

Na Moabu ataangamizwa, asiwe taifa tena, kwa sababu alijitukuza juu ya Bwana.

Yeremia 48:43 Jeremiah 48:43

Hofu, na shimo, na mtego, zaja juu yako, Ee mwenyeji wa Moabu, asema Bwana.

Yeremia 48:44 Jeremiah 48:44

Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema Bwana.

Yeremia 48:45 Jeremiah 48:45

Wamekimbia, wasio na nguvu Wanasimama chini ya kivuli cha Heshboni; Ila moto umetoka katika Heshboni, Na mwali wa moto toka kati ya Sihoni Nao umekula pembe ya Moabu, Na utosi wa kichwa wa watu wapigao kelele.

Yeremia 48:46 Jeremiah 48:46

Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani.

Yeremia 48:47 Jeremiah 48:47

Lakini nitawarudisha watu wa Moabu walio utumwani, siku za mwisho, asema Bwana. Hukumu ya Moabu imefikilia hapa.