Yeremia Mlango 27 Jeremiah

Yeremia 27:1 Jeremiah 27:1

Mwanzo wa kumiliki kwake Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,

Yeremia 27:2 Jeremiah 27:2

Bwana ameniambia hivi, Jifanyizie vifungo na nira, ukajivike shingoni;

Yeremia 27:3 Jeremiah 27:3

kisha uvipeleke kwa mfalme wa Edomu, na mfalme wa Moabu, na mfalme wa wana wa Amoni, na mfalme wa Tiro, na mfalme wa Sidoni, kwa mikono ya wajumbe watakaofika Yerusalemu kwa Sedekia, mfalme wa Yuda.

Yeremia 27:4 Jeremiah 27:4

Uwaagize waende kwa bwana zao, na kuwaambia, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Mtawaambia bwana zenu maneno haya;

Yeremia 27:5 Jeremiah 27:5

Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.

Yeremia 27:6 Jeremiah 27:6

Na sasa nimetia nchi hizi zote katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama wa mwituni pia nimempa wamtumikie.

Yeremia 27:7 Jeremiah 27:7

Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.

Yeremia 27:8 Jeremiah 27:8

Na itakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadreza, huyo mfalme wa Babeli, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema Bwana, hata nitakapokuwa nimewaangamiza kwa mkono wake.

Yeremia 27:9 Jeremiah 27:9

Lakini, katika habari zenu, msisikilize manabii wenu, wala wabashiri wenu, wala ndoto zenu, wala watambuzi wenu, wala waganga wenu, wanaowaambia, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli;

Yeremia 27:10 Jeremiah 27:10

maana wanawatabiria uongo, ili kuwatoa ninyi mbali na nchi yenu; niwafukuze mkaangamie.

Yeremia 27:11 Jeremiah 27:11

Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema Bwana; nao watailima, na kukaa ndani yake.

Yeremia 27:12 Jeremiah 27:12

Nikamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, kwa mfano wa maneno hayo yote, nikisema, Tieni shingo zenu katika nira ya mfalme wa Babeli, mkamtumikie yeye na watu wake, mpate kuishi.

Yeremia 27:13 Jeremiah 27:13

Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama Bwana alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli?

Yeremia 27:14 Jeremiah 27:14

Wala msisikilize maneno ya manabii wawaambiao ninyi, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli; maana wanawatabiria uongo.

Yeremia 27:15 Jeremiah 27:15

Kwa maana mimi sikuwatuma, asema Bwana, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria.

Yeremia 27:16 Jeremiah 27:16

Pia nalisema na makuhani, na watu wote, nikisema, Bwana asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya Bwana, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo.

Yeremia 27:17 Jeremiah 27:17

Msiwasikilize; mtumikieni mfalme wa Babeli, mkaishi; kwani mji huu kufanywa ukiwa?

Yeremia 27:18 Jeremiah 27:18

Lakini ikiwa hao ni manabii, na ikiwa neno la Bwana liko kwao, basi na wamwombe Bwana wa majeshi, kwamba vyombo vile vilivyosalia katika nyumba ya Bwana, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu, visiende Babeli.

Yeremia 27:19 Jeremiah 27:19

Maana Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari za nguzo, na katika habari za bahari, na katika habari za matako yake, na katika habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu,

Yeremia 27:20 Jeremiah 27:20

ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, hakuvichukua, hapo alipomchukua Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu mpaka Babeli, pamoja na wakuu wote wa Yuda, na Yerusalemu;

Yeremia 27:21 Jeremiah 27:21

naam, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Bwana, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu;

Yeremia 27:22 Jeremiah 27:22

Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijilia, asema Bwana; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.