Yeremia Mlango 52 Jeremiah

Yeremia 52:1 Jeremiah 52:1

Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja hapo alipoanza kumiliki; naye akamiliki miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna.

Yeremia 52:2 Jeremiah 52:2

Naye alitenda yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyatenda Yehoyakimu.

Yeremia 52:3 Jeremiah 52:3

Maana, kwa sababu ya hasira ya Bwana, mambo haya yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata akawaondosha wasiwe mbele za uso wake, naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.

Yeremia 52:4 Jeremiah 52:4

Ikawa, katika mwaka wa kenda wa kumiliki kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, juu ya Yerusalemu, akapanga hema zake juu yake; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.

Yeremia 52:5 Jeremiah 52:5

Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na mmoja wa mfalme Sedekia.

Yeremia 52:6 Jeremiah 52:6

Katika mwezi wa nne, siku ya kenda ya mwezi, njaa ilizidi sana ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.

Yeremia 52:7 Jeremiah 52:7

Ukuta wa mji ukabomolewa, watu wote wa vita wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji pande zote;) wakaenda zao kwa njia ya Araba.

Yeremia 52:8 Jeremiah 52:8

Lakini jeshi la Wakaldayo wakamfuatia mfalme, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko, na jeshi lake lote walikuwa wametawanyika na kumwacha.

Yeremia 52:9 Jeremiah 52:9

Nao wakamshika mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli, aliyekuwa huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.

Yeremia 52:10 Jeremiah 52:10

Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake; pia akawaua wakuu wote wa Yuda huko Ribla.

Yeremia 52:11 Jeremiah 52:11

Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake.

Yeremia 52:12 Jeremiah 52:12

Basi katika mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli; Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, aliyesimama mbele ya mfalme wa Babeli, aliingia Yerusalemu.

Yeremia 52:13 Jeremiah 52:13

Akaiteketeza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.

Yeremia 52:14 Jeremiah 52:14

Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo amiri wa askari walinzi, wakazibomoa kuta zote za Yerusalemu pande zote.

Yeremia 52:15 Jeremiah 52:15

Kisha Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua wafungwa baadhi ya watu waliokuwa maskini, na mabaki ya watu walioachwa katika mji, nao wale walioasi na kumkimbilia mfalme wa Babeli, nao mabaki ya vibarua.

Yeremia 52:16 Jeremiah 52:16

Lakini Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawaacha watu walio maskini kabisa ili wawe watunza mizabibu na wakulima.

Yeremia 52:17 Jeremiah 52:17

Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya Bwana, na matako ya bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Bwana, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.

Yeremia 52:18 Jeremiah 52:18

Nayo masufuria, na majembe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyombo vyote vya shaba walivyokuwa wakivitumia, wakavichukua vyote.

Yeremia 52:19 Jeremiah 52:19

Navyo vikombe, na vyombo vya kutolea majivu, na mabakuli, na masufuria, na vinara, na miiko, na vyetezo, vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, amiri wa askari walinzi akavichukua.

Yeremia 52:20 Jeremiah 52:20

Nguzo mbili, bahari moja, na ng'ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya matako yake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya Bwana; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.

Yeremia 52:21 Jeremiah 52:21

Na nguzo hizo, urefu wa nguzo moja ulikuwa dhiraa kumi na nane, na uzi wa dhiraa kumi na mbili ungeweza kuizunguka; na unene wake ulikuwa nyanda nne; nayo ilikuwa ya uvungu.

Yeremia 52:22 Jeremiah 52:22

Nayo ilikuwa na kichwa cha shaba juu yake; na urefu wa kichwa kimoja ulikuwa dhiraa tano; palikuwa na mapambo ya wavu na makomamanga juu ya kichwa hicho pande zote; vyote vilikuwa vya shaba; nayo nguzo ya pili ilikuwa na mapambo kama hayo, na makomamanga.

Yeremia 52:23 Jeremiah 52:23

Palikuwa na makomamanga tisini na sita katika pande zake; makomamanga; yote yalikuwa mia juu ya wavu huo pande zote.

Yeremia 52:24 Jeremiah 52:24

Naye amiri wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watatu wa mlango;

Yeremia 52:25 Jeremiah 52:25

na katika mji akatwaa towashi mmoja aliyewasimamia watu wa vita; na watu saba katika wale waliouona uso wa mfalme, walioonekana katika mji; na karani wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana ndani ya mji.

Yeremia 52:26 Jeremiah 52:26

Na Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawatwaa, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.

Yeremia 52:27 Jeremiah 52:27

Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Ndivyo Yuda alivyochukuliwa utumwani, akatolewa katika nchi yake.

Yeremia 52:28 Jeremiah 52:28

Watu hawa ndio wale ambao Nebukadreza aliwachukua mateka; katika mwaka wa saba, Wayahudi elfu tatu na ishirini na watatu;

Yeremia 52:29 Jeremiah 52:29

katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza aliwachukua toka Yerusalemu watu mia nane na thelathini na wawili;

Yeremia 52:30 Jeremiah 52:30

katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadreza, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.

Yeremia 52:31 Jeremiah 52:31

Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.

Yeremia 52:32 Jeremiah 52:32

Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli.

Yeremia 52:33 Jeremiah 52:33

Naye akabadili mavazi yake ya gerezani, akala chakula mbele yake daima, siku zote za maisha yake.

Yeremia 52:34 Jeremiah 52:34

Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme wa Babeli; kila siku alipewa posho hata siku ya kufa kwake, siku zote za maisha yake.