Mathayo Mlango 14 Matthew

Mathayo 14:1 Matthew 14:1

Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake,

Mathayo 14:2 Matthew 14:2

Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake.

Mathayo 14:3 Matthew 14:3

Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye.

Mathayo 14:4 Matthew 14:4

Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye.

Mathayo 14:5 Matthew 14:5

Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii.

Mathayo 14:6 Matthew 14:6

Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.

Mathayo 14:7 Matthew 14:7

Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba.

Mathayo 14:8 Matthew 14:8

Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.

Mathayo 14:9 Matthew 14:9

Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe;

Mathayo 14:10 Matthew 14:10

akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.

Mathayo 14:11 Matthew 14:11

Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye.

Mathayo 14:12 Matthew 14:12

Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.

Mathayo 14:13 Matthew 14:13

Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao.

Mathayo 14:14 Matthew 14:14

Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

Mathayo 14:15 Matthew 14:15

Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.

Mathayo 14:16 Matthew 14:16

Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.

Mathayo 14:17 Matthew 14:17

Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.

Mathayo 14:18 Matthew 14:18

Akasema, Nileteeni hapa.

Mathayo 14:19 Matthew 14:19

Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.

Mathayo 14:20 Matthew 14:20

Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.

Mathayo 14:21 Matthew 14:21

Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.

Mathayo 14:22 Matthew 14:22

Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.

Mathayo 14:23 Matthew 14:23

Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.

Mathayo 14:24 Matthew 14:24

Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.

Mathayo 14:25 Matthew 14:25

Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.

Mathayo 14:26 Matthew 14:26

Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.

Mathayo 14:27 Matthew 14:27

Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.

Mathayo 14:28 Matthew 14:28

Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

Mathayo 14:29 Matthew 14:29

Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

Mathayo 14:30 Matthew 14:30

Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

Mathayo 14:31 Matthew 14:31

Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Mathayo 14:32 Matthew 14:32

Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma.

Mathayo 14:33 Matthew 14:33

Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.

Mathayo 14:34 Matthew 14:34

Na walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti.

Mathayo 14:35 Matthew 14:35

Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi;

Mathayo 14:36 Matthew 14:36

nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.