Mathayo Mlango 16 Matthew

Mathayo 16:1 Matthew 16:1

Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni.

Mathayo 16:2 Matthew 16:2

Akajibu, akawaambia, [Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu.

Mathayo 16:3 Matthew 16:3

Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?]

Mathayo 16:4 Matthew 16:4

Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.

Mathayo 16:5 Matthew 16:5

Nao wanafunzi wakaenda hata ng'ambo, wakasahau kuchukua mikate.

Mathayo 16:6 Matthew 16:6

Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Mathayo 16:7 Matthew 16:7

Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.

Mathayo 16:8 Matthew 16:8

Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate?

Mathayo 16:9 Matthew 16:9

Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota?

Mathayo 16:10 Matthew 16:10

Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota?

Mathayo 16:11 Matthew 16:11

Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Mathayo 16:12 Matthew 16:12

Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Mathayo 16:13 Matthew 16:13

Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?

Mathayo 16:14 Matthew 16:14

Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.

Mathayo 16:15 Matthew 16:15

Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

Mathayo 16:16 Matthew 16:16

Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

Mathayo 16:17 Matthew 16:17

Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

Mathayo 16:18 Matthew 16:18

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

Mathayo 16:19 Matthew 16:19

Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Mathayo 16:20 Matthew 16:20

Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.

Mathayo 16:21 Matthew 16:21

Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

Mathayo 16:22 Matthew 16:22

Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.

Mathayo 16:23 Matthew 16:23

Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Mathayo 16:24 Matthew 16:24

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

Mathayo 16:25 Matthew 16:25

Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

Mathayo 16:26 Matthew 16:26

Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

Mathayo 16:27 Matthew 16:27

Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Mathayo 16:28 Matthew 16:28

Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.