Mathayo Mlango 1 Matthew

Mathayo 1:1 Matthew 1:1

Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.

Mathayo 1:2 Matthew 1:2

Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

Mathayo 1:3 Matthew 1:3

Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;

Mathayo 1:4 Matthew 1:4

Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;

Mathayo 1:5 Matthew 1:5

Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;

Mathayo 1:6 Matthew 1:6

Yese akamzaa mfalme Daudi.

Mathayo 1:7 Matthew 1:7

Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

Mathayo 1:8 Matthew 1:8

Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;

Mathayo 1:9 Matthew 1:9

Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;

Mathayo 1:10 Matthew 1:10

Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;

Mathayo 1:11 Matthew 1:11

Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

Mathayo 1:12 Matthew 1:12

Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;

Mathayo 1:13 Matthew 1:13

Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;

Mathayo 1:14 Matthew 1:14

Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;

Mathayo 1:15 Matthew 1:15

Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;

Mathayo 1:16 Matthew 1:16

Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

Mathayo 1:17 Matthew 1:17

Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.

Mathayo 1:18 Matthew 1:18

Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Mathayo 1:19 Matthew 1:19

Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

Mathayo 1:20 Matthew 1:20

Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Mathayo 1:21 Matthew 1:21

Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

Mathayo 1:22 Matthew 1:22

Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,

Mathayo 1:23 Matthew 1:23

Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.

Mathayo 1:24 Matthew 1:24

Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;

Mathayo 1:25 Matthew 1:25

asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.