Mathayo Mlango 24 Matthew

Mathayo 24:1 Matthew 24:1

Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu.

Mathayo 24:2 Matthew 24:2

Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.

Mathayo 24:3 Matthew 24:3

Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

Mathayo 24:4 Matthew 24:4

Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

Mathayo 24:5 Matthew 24:5

Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

Mathayo 24:6 Matthew 24:6

Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

Mathayo 24:7 Matthew 24:7

Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.

Mathayo 24:8 Matthew 24:8

Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.

Mathayo 24:9 Matthew 24:9

Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.

Mathayo 24:10 Matthew 24:10

Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.

Mathayo 24:11 Matthew 24:11

Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.

Mathayo 24:12 Matthew 24:12

Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.

Mathayo 24:13 Matthew 24:13

Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Mathayo 24:14 Matthew 24:14

Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Mathayo 24:15 Matthew 24:15

Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),

Mathayo 24:16 Matthew 24:16

ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;

Mathayo 24:17 Matthew 24:17

naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;

Mathayo 24:18 Matthew 24:18

wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.

Mathayo 24:19 Matthew 24:19

Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!

Mathayo 24:20 Matthew 24:20

Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.

Mathayo 24:21 Matthew 24:21

Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.

Mathayo 24:22 Matthew 24:22

Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.

Mathayo 24:23 Matthew 24:23

Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.

Mathayo 24:24 Matthew 24:24

Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

Mathayo 24:25 Matthew 24:25

Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

Mathayo 24:26 Matthew 24:26

Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.

Mathayo 24:27 Matthew 24:27

Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Mathayo 24:28 Matthew 24:28

Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

Mathayo 24:29 Matthew 24:29

Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;

Mathayo 24:30 Matthew 24:30

ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

Mathayo 24:31 Matthew 24:31

Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

Mathayo 24:32 Matthew 24:32

Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;

Mathayo 24:33 Matthew 24:33

nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.

Mathayo 24:34 Matthew 24:34

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.

Mathayo 24:35 Matthew 24:35

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Mathayo 24:36 Matthew 24:36

Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.

Mathayo 24:37 Matthew 24:37

Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Mathayo 24:38 Matthew 24:38

Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,

Mathayo 24:39 Matthew 24:39

wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Mathayo 24:40 Matthew 24:40

Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

Mathayo 24:41 Matthew 24:41

wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

Mathayo 24:42 Matthew 24:42

Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

Mathayo 24:43 Matthew 24:43

Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.

Mathayo 24:44 Matthew 24:44

Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.

Mathayo 24:45 Matthew 24:45

Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?

Mathayo 24:46 Matthew 24:46

Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.

Mathayo 24:47 Matthew 24:47

Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.

Mathayo 24:48 Matthew 24:48

Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;

Mathayo 24:49 Matthew 24:49

akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;

Mathayo 24:50 Matthew 24:50

bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,

Mathayo 24:51 Matthew 24:51

atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.