Mathayo Mlango 19 Matthew

Mathayo 19:1 Matthew 19:1

Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani.

Mathayo 19:2 Matthew 19:2

Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.

Mathayo 19:3 Matthew 19:3

Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

Mathayo 19:4 Matthew 19:4

Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

Mathayo 19:5 Matthew 19:5

akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Mathayo 19:6 Matthew 19:6

Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

Mathayo 19:7 Matthew 19:7

Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

Mathayo 19:8 Matthew 19:8

Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

Mathayo 19:9 Matthew 19:9

Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Mathayo 19:10 Matthew 19:10

Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

Mathayo 19:11 Matthew 19:11

Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.

Mathayo 19:12 Matthew 19:12

Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Mathayo 19:13 Matthew 19:13

Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.

Mathayo 19:14 Matthew 19:14

Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.

Mathayo 19:15 Matthew 19:15

Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.

Mathayo 19:16 Matthew 19:16

Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?

Mathayo 19:17 Matthew 19:17

Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.

Mathayo 19:18 Matthew 19:18

Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,

Mathayo 19:19 Matthew 19:19

Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Mathayo 19:20 Matthew 19:20

Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?

Mathayo 19:21 Matthew 19:21

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

Mathayo 19:22 Matthew 19:22

Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Mathayo 19:23 Matthew 19:23

Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Mathayo 19:24 Matthew 19:24

Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Mathayo 19:25 Matthew 19:25

Wanafunzi waliposikia, walishangaa mno, wakisema, Ni nani basi awezaye kuokoka?

Mathayo 19:26 Matthew 19:26

Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.

Mathayo 19:27 Matthew 19:27

Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?

Mathayo 19:28 Matthew 19:28

Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

Mathayo 19:29 Matthew 19:29

Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.

Mathayo 19:30 Matthew 19:30

Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.