Mathayo Mlango 22 Matthew

Mathayo 22:1 Matthew 22:1

Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema,

Mathayo 22:2 Matthew 22:2

Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.

Mathayo 22:3 Matthew 22:3

Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja.

Mathayo 22:4 Matthew 22:4

Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.

Mathayo 22:5 Matthew 22:5

Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake;

Mathayo 22:6 Matthew 22:6

nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua.

Mathayo 22:7 Matthew 22:7

Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.

Mathayo 22:8 Matthew 22:8

Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili.

Mathayo 22:9 Matthew 22:9

Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.

Mathayo 22:10 Matthew 22:10

Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.

Mathayo 22:11 Matthew 22:11

Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.

Mathayo 22:12 Matthew 22:12

Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.

Mathayo 22:13 Matthew 22:13

Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mathayo 22:14 Matthew 22:14

Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Mathayo 22:15 Matthew 22:15

Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno.

Mathayo 22:16 Matthew 22:16

Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu.

Mathayo 22:17 Matthew 22:17

Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo?

Mathayo 22:18 Matthew 22:18

Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki?

Mathayo 22:19 Matthew 22:19

Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari.

Mathayo 22:20 Matthew 22:20

Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii?

Mathayo 22:21 Matthew 22:21

Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.

Mathayo 22:22 Matthew 22:22

Waliposikia, walistaajabu, wakamwacha, wakaenda zao.

Mathayo 22:23 Matthew 22:23

Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,

Mathayo 22:24 Matthew 22:24

wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.

Mathayo 22:25 Matthew 22:25

Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.

Mathayo 22:26 Matthew 22:26

Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.

Mathayo 22:27 Matthew 22:27

Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

Mathayo 22:28 Matthew 22:28

Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.

Mathayo 22:29 Matthew 22:29

Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.

Mathayo 22:30 Matthew 22:30

Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.

Mathayo 22:31 Matthew 22:31

Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema,

Mathayo 22:32 Matthew 22:32

Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.

Mathayo 22:33 Matthew 22:33

Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.

Mathayo 22:34 Matthew 22:34

Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja.

Mathayo 22:35 Matthew 22:35

Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;

Mathayo 22:36 Matthew 22:36

Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?

Mathayo 22:37 Matthew 22:37

Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

Mathayo 22:38 Matthew 22:38

Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

Mathayo 22:39 Matthew 22:39

Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Mathayo 22:40 Matthew 22:40

Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Mathayo 22:41 Matthew 22:41

Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?

Mathayo 22:42 Matthew 22:42

Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

Mathayo 22:43 Matthew 22:43

Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,

Mathayo 22:44 Matthew 22:44

Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

Mathayo 22:45 Matthew 22:45

Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

Mathayo 22:46 Matthew 22:46

Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.