Mathayo Mlango 25 Matthew

Mathayo 25:1 Matthew 25:1

Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

Mathayo 25:2 Matthew 25:2

Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.

Mathayo 25:3 Matthew 25:3

Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

Mathayo 25:4 Matthew 25:4

bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

Mathayo 25:5 Matthew 25:5

Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

Mathayo 25:6 Matthew 25:6

Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

Mathayo 25:7 Matthew 25:7

Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

Mathayo 25:8 Matthew 25:8

Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

Mathayo 25:9 Matthew 25:9

Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.

Mathayo 25:10 Matthew 25:10

Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

Mathayo 25:11 Matthew 25:11

Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.

Mathayo 25:12 Matthew 25:12

Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.

Mathayo 25:13 Matthew 25:13

Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Mathayo 25:14 Matthew 25:14

Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.

Mathayo 25:15 Matthew 25:15

Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.

Mathayo 25:16 Matthew 25:16

Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.

Mathayo 25:17 Matthew 25:17

Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.

Mathayo 25:18 Matthew 25:18

Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.

Mathayo 25:19 Matthew 25:19

Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

Mathayo 25:20 Matthew 25:20

Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.

Mathayo 25:21 Matthew 25:21

Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

Mathayo 25:22 Matthew 25:22

Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.

Mathayo 25:23 Matthew 25:23

Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

Mathayo 25:24 Matthew 25:24

Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

Mathayo 25:25 Matthew 25:25

basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

Mathayo 25:26 Matthew 25:26

Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

Mathayo 25:27 Matthew 25:27

basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

Mathayo 25:28 Matthew 25:28

Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

Mathayo 25:29 Matthew 25:29

Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.

Mathayo 25:30 Matthew 25:30

Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mathayo 25:31 Matthew 25:31

Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

Mathayo 25:32 Matthew 25:32

na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

Mathayo 25:33 Matthew 25:33

atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

Mathayo 25:34 Matthew 25:34

Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

Mathayo 25:35 Matthew 25:35

kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

Mathayo 25:36 Matthew 25:36

nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

Mathayo 25:37 Matthew 25:37

Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

Mathayo 25:38 Matthew 25:38

Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

Mathayo 25:39 Matthew 25:39

Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

Mathayo 25:40 Matthew 25:40

Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

Mathayo 25:41 Matthew 25:41

Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

Mathayo 25:42 Matthew 25:42

kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

Mathayo 25:43 Matthew 25:43

nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

Mathayo 25:44 Matthew 25:44

Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

Mathayo 25:45 Matthew 25:45

Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

Mathayo 25:46 Matthew 25:46

Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.