Mathayo Mlango 11 Matthew

Mathayo 11:1 Matthew 11:1

Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

Mathayo 11:2 Matthew 11:2

Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,

Mathayo 11:3 Matthew 11:3

Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

Mathayo 11:4 Matthew 11:4

Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;

Mathayo 11:5 Matthew 11:5

vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.

Mathayo 11:6 Matthew 11:6

Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.

Mathayo 11:7 Matthew 11:7

Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?

Mathayo 11:8 Matthew 11:8

Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme.

Mathayo 11:9 Matthew 11:9

Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii.

Mathayo 11:10 Matthew 11:10

Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.

Mathayo 11:11 Matthew 11:11

Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.

Mathayo 11:12 Matthew 11:12

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Mathayo 11:13 Matthew 11:13

Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.

Mathayo 11:14 Matthew 11:14

Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.

Mathayo 11:15 Matthew 11:15

Mwenye masikio, na asikie.

Mathayo 11:16 Matthew 11:16

Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,

Mathayo 11:17 Matthew 11:17

Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.

Mathayo 11:18 Matthew 11:18

Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.

Mathayo 11:19 Matthew 11:19

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

Mathayo 11:20 Matthew 11:20

Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.

Mathayo 11:21 Matthew 11:21

Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.

Mathayo 11:22 Matthew 11:22

Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

Mathayo 11:23 Matthew 11:23

Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.

Mathayo 11:24 Matthew 11:24

Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.

Mathayo 11:25 Matthew 11:25

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.

Mathayo 11:26 Matthew 11:26

Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Mathayo 11:27 Matthew 11:27

Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

Mathayo 11:28 Matthew 11:28

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Mathayo 11:29 Matthew 11:29

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

Mathayo 11:30 Matthew 11:30

kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.