Mathayo Mlango 9 Matthew

Mathayo 9:1 Matthew 9:1

Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao.

Mathayo 9:2 Matthew 9:2

Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

Mathayo 9:3 Matthew 9:3

Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.

Mathayo 9:4 Matthew 9:4

Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?

Mathayo 9:5 Matthew 9:5

Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende?

Mathayo 9:6 Matthew 9:6

Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.

Mathayo 9:7 Matthew 9:7

Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.

Mathayo 9:8 Matthew 9:8

Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.

Mathayo 9:9 Matthew 9:9

Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.

Mathayo 9:10 Matthew 9:10

Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.

Mathayo 9:11 Matthew 9:11

Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

Mathayo 9:12 Matthew 9:12

Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

Mathayo 9:13 Matthew 9:13

Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Mathayo 9:14 Matthew 9:14

Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?

Mathayo 9:15 Matthew 9:15

Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.

Mathayo 9:16 Matthew 9:16

Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.

Mathayo 9:17 Matthew 9:17

Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.

Mathayo 9:18 Matthew 9:18

Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.

Mathayo 9:19 Matthew 9:19

Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.

Mathayo 9:20 Matthew 9:20

Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.

Mathayo 9:21 Matthew 9:21

Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.

Mathayo 9:22 Matthew 9:22

Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

Mathayo 9:23 Matthew 9:23

Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,

Mathayo 9:24 Matthew 9:24

akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.

Mathayo 9:25 Matthew 9:25

Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama.

Mathayo 9:26 Matthew 9:26

Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote.

Mathayo 9:27 Matthew 9:27

Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.

Mathayo 9:28 Matthew 9:28

Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana.

Mathayo 9:29 Matthew 9:29

Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.

Mathayo 9:30 Matthew 9:30

Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue.

Mathayo 9:31 Matthew 9:31

Lakini wakatoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote.

Mathayo 9:32 Matthew 9:32

Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.

Mathayo 9:33 Matthew 9:33

Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.

Mathayo 9:34 Matthew 9:34

Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.

Mathayo 9:35 Matthew 9:35

Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

Mathayo 9:36 Matthew 9:36

Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.

Mathayo 9:37 Matthew 9:37

Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.

Mathayo 9:38 Matthew 9:38

Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.