Mathayo Mlango 8 Matthew

Mathayo 8:1 Matthew 8:1

Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.

Mathayo 8:2 Matthew 8:2

Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.

Mathayo 8:3 Matthew 8:3

Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.

Mathayo 8:4 Matthew 8:4

Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

Mathayo 8:5 Matthew 8:5

Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

Mathayo 8:6 Matthew 8:6

akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

Mathayo 8:7 Matthew 8:7

Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

Mathayo 8:8 Matthew 8:8

Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

Mathayo 8:9 Matthew 8:9

Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

Mathayo 8:10 Matthew 8:10

Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.

Mathayo 8:11 Matthew 8:11

Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;

Mathayo 8:12 Matthew 8:12

bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mathayo 8:13 Matthew 8:13

Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.

Mathayo 8:14 Matthew 8:14

Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa.

Mathayo 8:15 Matthew 8:15

Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia.

Mathayo 8:16 Matthew 8:16

Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,

Mathayo 8:17 Matthew 8:17

ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

Mathayo 8:18 Matthew 8:18

Naye Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng'ambo.

Mathayo 8:19 Matthew 8:19

Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako.

Mathayo 8:20 Matthew 8:20

Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.

Mathayo 8:21 Matthew 8:21

Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu.

Mathayo 8:22 Matthew 8:22

Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.

Mathayo 8:23 Matthew 8:23

Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata.

Mathayo 8:24 Matthew 8:24

Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.

Mathayo 8:25 Matthew 8:25

Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.

Mathayo 8:26 Matthew 8:26

Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.

Mathayo 8:27 Matthew 8:27

Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?

Mathayo 8:28 Matthew 8:28

Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.

Mathayo 8:29 Matthew 8:29

Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

Mathayo 8:30 Matthew 8:30

Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.

Mathayo 8:31 Matthew 8:31

Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.

Mathayo 8:32 Matthew 8:32

Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.

Mathayo 8:33 Matthew 8:33

Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.

Mathayo 8:34 Matthew 8:34

Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.