Mathayo Mlango 12 Matthew

Mathayo 12:1 Matthew 12:1

Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.

Mathayo 12:2 Matthew 12:2

Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.

Mathayo 12:3 Matthew 12:3

Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe?

Mathayo 12:4 Matthew 12:4

jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?

Mathayo 12:5 Matthew 12:5

Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?

Mathayo 12:6 Matthew 12:6

Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.

Mathayo 12:7 Matthew 12:7

Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.

Mathayo 12:8 Matthew 12:8

Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

Mathayo 12:9 Matthew 12:9

Akaondoka huko, akaingia katika sinagogi lao.

Mathayo 12:10 Matthew 12:10

Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza; wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? Wapate kumshitaki.

Mathayo 12:11 Matthew 12:11

Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa?

Mathayo 12:12 Matthew 12:12

Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.

Mathayo 12:13 Matthew 12:13

Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili.

Mathayo 12:14 Matthew 12:14

Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.

Mathayo 12:15 Matthew 12:15

Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,

Mathayo 12:16 Matthew 12:16

akawakataza wasimdhihirishe;

Mathayo 12:17 Matthew 12:17

ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

Mathayo 12:18 Matthew 12:18

Tazama, mtumishi wangu niliyemteua; Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye; Nitatia roho yangu juu yake, Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

Mathayo 12:19 Matthew 12:19

Hatateta wala hatapaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.

Mathayo 12:20 Matthew 12:20

Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.

Mathayo 12:21 Matthew 12:21

Na jina lake Mataifa watalitumainia.

Mathayo 12:22 Matthew 12:22

Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.

Mathayo 12:23 Matthew 12:23

Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?

Mathayo 12:24 Matthew 12:24

Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.

Mathayo 12:25 Matthew 12:25

Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.

Mathayo 12:26 Matthew 12:26

Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?

Mathayo 12:27 Matthew 12:27

Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.

Mathayo 12:28 Matthew 12:28

Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.

Mathayo 12:29 Matthew 12:29

Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.

Mathayo 12:30 Matthew 12:30

Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

Mathayo 12:31 Matthew 12:31

Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.

Mathayo 12:32 Matthew 12:32

Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

Mathayo 12:33 Matthew 12:33

Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.

Mathayo 12:34 Matthew 12:34

Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.

Mathayo 12:35 Matthew 12:35

Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.

Mathayo 12:36 Matthew 12:36

Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

Mathayo 12:37 Matthew 12:37

Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Mathayo 12:38 Matthew 12:38

Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.

Mathayo 12:39 Matthew 12:39

Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.

Mathayo 12:40 Matthew 12:40

Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.

Mathayo 12:41 Matthew 12:41

Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

Mathayo 12:42 Matthew 12:42

Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

Mathayo 12:43 Matthew 12:43

Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

Mathayo 12:44 Matthew 12:44

Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

Mathayo 12:45 Matthew 12:45

Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.

Mathayo 12:46 Matthew 12:46

Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.

Mathayo 12:47 Matthew 12:47

Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.

Mathayo 12:48 Matthew 12:48

Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?

Mathayo 12:49 Matthew 12:49

Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!

Mathayo 12:50 Matthew 12:50

Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.