Mathayo Mlango 20 Matthew

Mathayo 20:1 Matthew 20:1

Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.

Mathayo 20:2 Matthew 20:2

Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.

Mathayo 20:3 Matthew 20:3

Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;

Mathayo 20:4 Matthew 20:4

na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.

Mathayo 20:5 Matthew 20:5

Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.

Mathayo 20:6 Matthew 20:6

Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?

Mathayo 20:7 Matthew 20:7

Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.

Mathayo 20:8 Matthew 20:8

Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza.

Mathayo 20:9 Matthew 20:9

Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.

Mathayo 20:10 Matthew 20:10

Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.

Mathayo 20:11 Matthew 20:11

Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba,

Mathayo 20:12 Matthew 20:12

wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.

Mathayo 20:13 Matthew 20:13

Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

Mathayo 20:14 Matthew 20:14

Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

Mathayo 20:15 Matthew 20:15

Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

Mathayo 20:16 Matthew 20:16

Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.

Mathayo 20:17 Matthew 20:17

Hata Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia,

Mathayo 20:18 Matthew 20:18

Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi; nao watamhukumu afe;

Mathayo 20:19 Matthew 20:19

kisha watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibisha; na siku ya tatu atafufuka.

Mathayo 20:20 Matthew 20:20

Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.

Mathayo 20:21 Matthew 20:21

Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

Mathayo 20:22 Matthew 20:22

Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.

Mathayo 20:23 Matthew 20:23

Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.

Mathayo 20:24 Matthew 20:24

Na wale kumi waliposikia, waliwakasirikia wale ndugu wawili.

Mathayo 20:25 Matthew 20:25

Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

Mathayo 20:26 Matthew 20:26

Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;

Mathayo 20:27 Matthew 20:27

na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;

Mathayo 20:28 Matthew 20:28

kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

Mathayo 20:29 Matthew 20:29

Hata walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata.

Mathayo 20:30 Matthew 20:30

Na tazama, vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!

Mathayo 20:31 Matthew 20:31

Mkutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!

Mathayo 20:32 Matthew 20:32

Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini?

Mathayo 20:33 Matthew 20:33

Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe.

Mathayo 20:34 Matthew 20:34

Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata.