Mathayo Mlango 3 Matthew

Mathayo 3:1 Matthew 3:1

Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,

Mathayo 3:2 Matthew 3:2

Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Mathayo 3:3 Matthew 3:3

Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.

Mathayo 3:4 Matthew 3:4

Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.

Mathayo 3:5 Matthew 3:5

Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;

Mathayo 3:6 Matthew 3:6

naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.

Mathayo 3:7 Matthew 3:7

Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?

Mathayo 3:8 Matthew 3:8

Basi zaeni matunda yapasayo toba;

Mathayo 3:9 Matthew 3:9

wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.

Mathayo 3:10 Matthew 3:10

Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

Mathayo 3:11 Matthew 3:11

Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Mathayo 3:12 Matthew 3:12

Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.

Mathayo 3:13 Matthew 3:13

Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.

Mathayo 3:14 Matthew 3:14

Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?

Mathayo 3:15 Matthew 3:15

Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.

Mathayo 3:16 Matthew 3:16

Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

Mathayo 3:17 Matthew 3:17

na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.