Mathayo Mlango 5 Matthew

Mathayo 5:1 Matthew 5:1

Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;

Mathayo 5:2 Matthew 5:2

akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,

Mathayo 5:3 Matthew 5:3

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Mathayo 5:4 Matthew 5:4

Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

Mathayo 5:5 Matthew 5:5

Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.

Mathayo 5:6 Matthew 5:6

Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Mathayo 5:7 Matthew 5:7

Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

Mathayo 5:8 Matthew 5:8

Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Mathayo 5:9 Matthew 5:9

Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Mathayo 5:10 Matthew 5:10

Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Mathayo 5:11 Matthew 5:11

Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.

Mathayo 5:12 Matthew 5:12

Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Mathayo 5:13 Matthew 5:13

Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Mathayo 5:14 Matthew 5:14

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.

Mathayo 5:15 Matthew 5:15

Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.

Mathayo 5:16 Matthew 5:16

Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Mathayo 5:17 Matthew 5:17

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

Mathayo 5:18 Matthew 5:18

Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.

Mathayo 5:19 Matthew 5:19

Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Mathayo 5:20 Matthew 5:20

Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Mathayo 5:21 Matthew 5:21

Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

Mathayo 5:22 Matthew 5:22

Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Mathayo 5:23 Matthew 5:23

Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

Mathayo 5:24 Matthew 5:24

iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

Mathayo 5:25 Matthew 5:25

Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.

Mathayo 5:26 Matthew 5:26

Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

Mathayo 5:27 Matthew 5:27

Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;

Mathayo 5:28 Matthew 5:28

lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Mathayo 5:29 Matthew 5:29

Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

Mathayo 5:30 Matthew 5:30

Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

Mathayo 5:31 Matthew 5:31

Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;

Mathayo 5:32 Matthew 5:32

lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Mathayo 5:33 Matthew 5:33

Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;

Mathayo 5:34 Matthew 5:34

lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;

Mathayo 5:35 Matthew 5:35

wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

Mathayo 5:36 Matthew 5:36

Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.

Mathayo 5:37 Matthew 5:37

Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Mathayo 5:38 Matthew 5:38

Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;

Mathayo 5:39 Matthew 5:39

Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

Mathayo 5:40 Matthew 5:40

Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.

Mathayo 5:41 Matthew 5:41

Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.

Mathayo 5:42 Matthew 5:42

Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Mathayo 5:43 Matthew 5:43

Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

Mathayo 5:44 Matthew 5:44

lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

Mathayo 5:45 Matthew 5:45

ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Mathayo 5:46 Matthew 5:46

Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

Mathayo 5:47 Matthew 5:47

Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

Mathayo 5:48 Matthew 5:48

Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.