Mathayo Mlango 28 Matthew

Mathayo 28:1 Matthew 28:1

Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.

Mathayo 28:2 Matthew 28:2

Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.

Mathayo 28:3 Matthew 28:3

Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.

Mathayo 28:4 Matthew 28:4

Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu.

Mathayo 28:5 Matthew 28:5

Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.

Mathayo 28:6 Matthew 28:6

Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.

Mathayo 28:7 Matthew 28:7

Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.

Mathayo 28:8 Matthew 28:8

Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari.

Mathayo 28:9 Matthew 28:9

Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.

Mathayo 28:10 Matthew 28:10

Kisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.

Mathayo 28:11 Matthew 28:11

Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.

Mathayo 28:12 Matthew 28:12

Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,

Mathayo 28:13 Matthew 28:13

wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.

Mathayo 28:14 Matthew 28:14

Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.

Mathayo 28:15 Matthew 28:15

Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.

Mathayo 28:16 Matthew 28:16

Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.

Mathayo 28:17 Matthew 28:17

Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.

Mathayo 28:18 Matthew 28:18

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

Mathayo 28:19 Matthew 28:19

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Mathayo 28:20 Matthew 28:20

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.