Mathayo Mlango 15 Matthew

Mathayo 15:1 Matthew 15:1

Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema,

Mathayo 15:2 Matthew 15:2

Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.

Mathayo 15:3 Matthew 15:3

Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?

Mathayo 15:4 Matthew 15:4

Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.

Mathayo 15:5 Matthew 15:5

Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,

Mathayo 15:6 Matthew 15:6

basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

Mathayo 15:7 Matthew 15:7

Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,

Mathayo 15:8 Matthew 15:8

Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.

Mathayo 15:9 Matthew 15:9

Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Mathayo 15:10 Matthew 15:10

Akawaita makutano akawaambia

Mathayo 15:11 Matthew 15:11

Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.

Mathayo 15:12 Matthew 15:12

Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?

Mathayo 15:13 Matthew 15:13

Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.

Mathayo 15:14 Matthew 15:14

Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Mathayo 15:15 Matthew 15:15

Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.

Mathayo 15:16 Matthew 15:16

Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?

Mathayo 15:17 Matthew 15:17

Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?

Mathayo 15:18 Matthew 15:18

Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

Mathayo 15:19 Matthew 15:19

Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

Mathayo 15:20 Matthew 15:20

hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.

Mathayo 15:21 Matthew 15:21

Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.

Mathayo 15:22 Matthew 15:22

Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.

Mathayo 15:23 Matthew 15:23

Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.

Mathayo 15:24 Matthew 15:24

Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Mathayo 15:25 Matthew 15:25

Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.

Mathayo 15:26 Matthew 15:26

Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

Mathayo 15:27 Matthew 15:27

Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.

Mathayo 15:28 Matthew 15:28

Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Mathayo 15:29 Matthew 15:29

Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.

Mathayo 15:30 Matthew 15:30

Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;

Mathayo 15:31 Matthew 15:31

hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Mathayo 15:32 Matthew 15:32

Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia njiani.

Mathayo 15:33 Matthew 15:33

Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?

Mathayo 15:34 Matthew 15:34

Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.

Mathayo 15:35 Matthew 15:35

Akawaagiza mkutano waketi chini;

Mathayo 15:36 Matthew 15:36

akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.

Mathayo 15:37 Matthew 15:37

Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.

Mathayo 15:38 Matthew 15:38

Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto.

Mathayo 15:39 Matthew 15:39

Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magadani.