Mwanzo Mlango 5 Genesis

Mwanzo 5:1 Genesis 5:1

Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;

Mwanzo 5:2 Genesis 5:2

mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.

Mwanzo 5:3 Genesis 5:3

Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.

Mwanzo 5:4 Genesis 5:4

Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:5 Genesis 5:5

Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.

Mwanzo 5:6 Genesis 5:6

Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.

Mwanzo 5:7 Genesis 5:7

Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:8 Genesis 5:8

Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.

Mwanzo 5:9 Genesis 5:9

Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.

Mwanzo 5:10 Genesis 5:10

Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:11 Genesis 5:11

Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.

Mwanzo 5:12 Genesis 5:12

Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.

Mwanzo 5:13 Genesis 5:13

Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:14 Genesis 5:14

Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.

Mwanzo 5:15 Genesis 5:15

Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.

Mwanzo 5:16 Genesis 5:16

Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:17 Genesis 5:17

Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.

Mwanzo 5:18 Genesis 5:18

Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.

Mwanzo 5:19 Genesis 5:19

Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:20 Genesis 5:20

Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.

Mwanzo 5:21 Genesis 5:21

Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.

Mwanzo 5:22 Genesis 5:22

Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:23 Genesis 5:23

Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.

Mwanzo 5:24 Genesis 5:24

Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.

Mwanzo 5:25 Genesis 5:25

Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.

Mwanzo 5:26 Genesis 5:26

Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:27 Genesis 5:27

Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.

Mwanzo 5:28 Genesis 5:28

Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.

Mwanzo 5:29 Genesis 5:29

Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.

Mwanzo 5:30 Genesis 5:30

Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 5:31 Genesis 5:31

Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.

Mwanzo 5:32 Genesis 5:32

Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.