Mwanzo Mlango 18 Genesis

Mwanzo 18:1 Genesis 18:1

Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.

Mwanzo 18:2 Genesis 18:2

Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,

Mwanzo 18:3 Genesis 18:3

akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.

Mwanzo 18:4 Genesis 18:4

Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.

Mwanzo 18:5 Genesis 18:5

Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.

Mwanzo 18:6 Genesis 18:6

Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.

Mwanzo 18:7 Genesis 18:7

Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.

Mwanzo 18:8 Genesis 18:8

Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.

Mwanzo 18:9 Genesis 18:9

Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.

Mwanzo 18:10 Genesis 18:10

Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

Mwanzo 18:11 Genesis 18:11

Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.

Mwanzo 18:12 Genesis 18:12

Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?

Mwanzo 18:13 Genesis 18:13

Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?

Mwanzo 18:14 Genesis 18:14

Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.

Mwanzo 18:15 Genesis 18:15

Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.

Mwanzo 18:16 Genesis 18:16

Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.

Mwanzo 18:17 Genesis 18:17

Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,

Mwanzo 18:18 Genesis 18:18

akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?

Mwanzo 18:19 Genesis 18:19

Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.

Mwanzo 18:20 Genesis 18:20

Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,

Mwanzo 18:21 Genesis 18:21

basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.

Mwanzo 18:22 Genesis 18:22

Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.

Mwanzo 18:23 Genesis 18:23

Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?

Mwanzo 18:24 Genesis 18:24

Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?

Mwanzo 18:25 Genesis 18:25

Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

Mwanzo 18:26 Genesis 18:26

Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.

Mwanzo 18:27 Genesis 18:27

Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.

Mwanzo 18:28 Genesis 18:28

Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.

Mwanzo 18:29 Genesis 18:29

Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.

Mwanzo 18:30 Genesis 18:30

Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.

Mwanzo 18:31 Genesis 18:31

Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.

Mwanzo 18:32 Genesis 18:32

Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

Mwanzo 18:33 Genesis 18:33

Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.