Mwanzo Mlango 15 Genesis

Mwanzo 15:1 Genesis 15:1

Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.

Mwanzo 15:2 Genesis 15:2

Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?

Mwanzo 15:3 Genesis 15:3

Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.

Mwanzo 15:4 Genesis 15:4

Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.

Mwanzo 15:5 Genesis 15:5

Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Mwanzo 15:6 Genesis 15:6

Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.

Mwanzo 15:7 Genesis 15:7

Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.

Mwanzo 15:8 Genesis 15:8

Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?

Mwanzo 15:9 Genesis 15:9

Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.

Mwanzo 15:10 Genesis 15:10

Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.

Mwanzo 15:11 Genesis 15:11

Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza.

Mwanzo 15:12 Genesis 15:12

Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.

Mwanzo 15:13 Genesis 15:13

Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.

Mwanzo 15:14 Genesis 15:14

Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.

Mwanzo 15:15 Genesis 15:15

Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.

Mwanzo 15:16 Genesis 15:16

Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.

Mwanzo 15:17 Genesis 15:17

Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.

Mwanzo 15:18 Genesis 15:18

Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

Mwanzo 15:19 Genesis 15:19

Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,

Mwanzo 15:20 Genesis 15:20

na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,

Mwanzo 15:21 Genesis 15:21

na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.