Mwanzo Mlango 27 Genesis

Mwanzo 27:1 Genesis 27:1

Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.

Mwanzo 27:2 Genesis 27:2

Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.

Mwanzo 27:3 Genesis 27:3

Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;

Mwanzo 27:4 Genesis 27:4

ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.

Mwanzo 27:5 Genesis 27:5

Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.

Mwanzo 27:6 Genesis 27:6

Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena,

Mwanzo 27:7 Genesis 27:7

Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za Bwana kabla ya kufa kwangu.

Mwanzo 27:8 Genesis 27:8

Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza.

Mwanzo 27:9 Genesis 27:9

Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo.

Mwanzo 27:10 Genesis 27:10

Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake.

Mwanzo 27:11 Genesis 27:11

Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini.

Mwanzo 27:12 Genesis 27:12

Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka.

Mwanzo 27:13 Genesis 27:13

Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee wana-mbuzi.

Mwanzo 27:14 Genesis 27:14

Akaenda, akawatwaa, akamletea mamaye. Mamaye akafanya chakula kitamu namna ile aliyopenda babaye.

Mwanzo 27:15 Genesis 27:15

Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo.

Mwanzo 27:16 Genesis 27:16

Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake.

Mwanzo 27:17 Genesis 27:17

Naye akampa Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu, na mkate alioufanya.

Mwanzo 27:18 Genesis 27:18

Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?

Mwanzo 27:19 Genesis 27:19

Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondoka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki.

Mwanzo 27:20 Genesis 27:20

Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu Bwana, Mungu wako, amenifanikisha.

Mwanzo 27:21 Genesis 27:21

Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo.

Mwanzo 27:22 Genesis 27:22

Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau.

Mwanzo 27:23 Genesis 27:23

Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki.

Mwanzo 27:24 Genesis 27:24

Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi.

Mwanzo 27:25 Genesis 27:25

Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa.

Mwanzo 27:26 Genesis 27:26

Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu.

Mwanzo 27:27 Genesis 27:27

Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.

Mwanzo 27:28 Genesis 27:28

Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo.

Mwanzo 27:29 Genesis 27:29

Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.

Mwanzo 27:30 Genesis 27:30

Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.

Mwanzo 27:31 Genesis 27:31

Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki.

Mwanzo 27:32 Genesis 27:32

Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.

Mwanzo 27:33 Genesis 27:33

Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.

Mwanzo 27:34 Genesis 27:34

Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.

Mwanzo 27:35 Genesis 27:35

Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.

Mwanzo 27:36 Genesis 27:36

Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?

Mwanzo 27:37 Genesis 27:37

Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu?

Mwanzo 27:38 Genesis 27:38

Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.

Mwanzo 27:39 Genesis 27:39

Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia,penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.

Mwanzo 27:40 Genesis 27:40

Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.

Mwanzo 27:41 Genesis 27:41

Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.

Mwanzo 27:42 Genesis 27:42

Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua.

Mwanzo 27:43 Genesis 27:43

Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani;

Mwanzo 27:44 Genesis 27:44

ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke;

Mwanzo 27:45 Genesis 27:45

hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?

Mwanzo 27:46 Genesis 27:46

Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?