Mwanzo Mlango 9 Genesis

Mwanzo 9:1 Genesis 9:1

Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.

Mwanzo 9:2 Genesis 9:2

Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.

Mwanzo 9:3 Genesis 9:3

Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.

Mwanzo 9:4 Genesis 9:4

Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

Mwanzo 9:5 Genesis 9:5

Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.

Mwanzo 9:6 Genesis 9:6

Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.

Mwanzo 9:7 Genesis 9:7

Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.

Mwanzo 9:8 Genesis 9:8

Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,

Mwanzo 9:9 Genesis 9:9

Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;

Mwanzo 9:10 Genesis 9:10

tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.

Mwanzo 9:11 Genesis 9:11

Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.

Mwanzo 9:12 Genesis 9:12

Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;

Mwanzo 9:13 Genesis 9:13

Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

Mwanzo 9:14 Genesis 9:14

Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,

Mwanzo 9:15 Genesis 9:15

nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.

Mwanzo 9:16 Genesis 9:16

Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.

Mwanzo 9:17 Genesis 9:17

Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.

Mwanzo 9:18 Genesis 9:18

Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.

Mwanzo 9:19 Genesis 9:19

Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.

Mwanzo 9:20 Genesis 9:20

Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

Mwanzo 9:21 Genesis 9:21

akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

Mwanzo 9:22 Genesis 9:22

Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

Mwanzo 9:23 Genesis 9:23

Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

Mwanzo 9:24 Genesis 9:24

Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

Mwanzo 9:25 Genesis 9:25

Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

Mwanzo 9:26 Genesis 9:26

Akasema,Na atukuzwe Bwana,Mungu wa Shemu;Na kaanani awe mtumwa wake.

Mwanzo 9:27 Genesis 9:27

Mungu akamnafisishe Yafethi,Na akae katika hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake.

Mwanzo 9:28 Genesis 9:28

Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.

Mwanzo 9:29 Genesis 9:29

Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.