Mwanzo Mlango 23 Genesis

Mwanzo 23:1 Genesis 23:1

Basi umri wake Sara ulikuwa miaka mia na ishirini na saba ndio umri wake Sara.

Mwanzo 23:2 Genesis 23:2

Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Ibrahimu akaja kumlilia Sara na kumwombolezea.

Mwanzo 23:3 Genesis 23:3

Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake, akasema na wazawa wa Hethi, akinena,

Mwanzo 23:4 Genesis 23:4

Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.

Mwanzo 23:5 Genesis 23:5

Wazawa wa Hethi wakamjibu Ibrahimu, wakamwambia,

Mwanzo 23:6 Genesis 23:6

Utusikie, Ee bwana, ndiwe mtu mkuu sana kwetu, uzike maiti wako katika kaburi lile utakalochagua katika makaburi yetu. Hapana mtu kwetu atakayekuzuilia kaburi lake, usizike maiti wako.

Mwanzo 23:7 Genesis 23:7

Ibrahimu akaondoka, akainama mbele ya watu wa nchi, mbele ya hao wazawa wa Hethi.

Mwanzo 23:8 Genesis 23:8

Naye akazungumza nao, akisema, Ikiwa nia yenu nimzike maiti wangu atoke mbele yangu, mnisikie, mkaniombee kwa Efroni bin Sohari,

Mwanzo 23:9 Genesis 23:9

ili kwamba anipe pango ya Makpela, iliyo katika mpaka wa shamba lake, na anipe kwa kima kilicho kamili, katikati yenu, iwe milki yangu ya kuzikia.

Mwanzo 23:10 Genesis 23:10

Basi Efroni alikuwa akiketi kati ya wazawa wa Hethi. Efroni Mhiti akamjibu Ibrahimu, na wazawa wa Hethi wanasikiliza, hata watu wote waingiao mlango wa mji wake, akisema,

Mwanzo 23:11 Genesis 23:11

Sivyo, bwana wangu, unisikilize. Lile shamba nakupa, na pango iliyomo nakupa; mbele ya wana wa watu wangu nakupa, uzike maiti wako.

Mwanzo 23:12 Genesis 23:12

Ibrahimu akainama mbele ya watu wa nchi.

Mwanzo 23:13 Genesis 23:13

Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu.

Mwanzo 23:14 Genesis 23:14

Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia,

Mwanzo 23:15 Genesis 23:15

Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n'nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.

Mwanzo 23:16 Genesis 23:16

Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.

Mwanzo 23:17 Genesis 23:17

Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango iliyokuwamo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa

Mwanzo 23:18 Genesis 23:18

kuwa mali yake Ibrahimu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.

Mwanzo 23:19 Genesis 23:19

Basi baada ya hayo Ibrahimu akamzika Sara mkewe katika pango ya shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.

Mwanzo 23:20 Genesis 23:20

Na lile shamba, na pango iliyomo, iliyakinishwa kuwa mali yake Ibrahimu na wazawa wa Hethi, kuwa mahali pa kuzikia.