Mwanzo Mlango 43 Genesis

Mwanzo 43:1 Genesis 43:1

Njaa ikawa nzito katika nchi.

Mwanzo 43:2 Genesis 43:2

Ikawa walipokwisha kula nafaka waliyoileta kutoka Misri, baba yao akawaambia, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo.

Mwanzo 43:3 Genesis 43:3

Yuda akamwambia akisema, Yule mtu alituagizia sana akisema, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi.

Mwanzo 43:4 Genesis 43:4

Ukimpeleka ndugu yetu pamoja nasi, tutashuka na kukununulia chakula.

Mwanzo 43:5 Genesis 43:5

Ila usipompeleka, hatushuki, maana mtu yule alituambia, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi.

Mwanzo 43:6 Genesis 43:6

Israeli akasema, Mbona mmenitendea vibaya hata mkamwarifu mtu yule ya kwamba mna ndugu mwingine?

Mwanzo 43:7 Genesis 43:7

Wakasema, Mtu yule alituhoji sana habari zetu na za jamaa yetu, akisema, Baba yenu angali hai? Mnaye ndugu mwingine? Nasi tukamjibu sawasawa na maswali hayo. Je! Tuliweza kujua ya kwamba atasema, Shukeni pamoja na ndugu yenu?

Mwanzo 43:8 Genesis 43:8

Yuda akamwambia Israeli babaye, Mpeleke kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu.

Mwanzo 43:9 Genesis 43:9

Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;

Mwanzo 43:10 Genesis 43:10

maana kama hatungalikawia, hakika tungaliisha kurudi mara ya pili.

Mwanzo 43:11 Genesis 43:11

Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.

Mwanzo 43:12 Genesis 43:12

Mkatwae fedha maradufu mikononi mwenu, na fedha zile zilizorudishwa kinywani mwa magunia yenu zirudisheni mikononi mwenu; labda zilisahauliwa.

Mwanzo 43:13 Genesis 43:13

Mtwaeni na ndugu yenu, mwondoke na kurudi kwa mtu yule.

Mwanzo 43:14 Genesis 43:14

Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.

Mwanzo 43:15 Genesis 43:15

Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu.

Mwanzo 43:16 Genesis 43:16

Naye Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, Uwalete watu hawa nyumbani, ukachinje na kuandalia, maana watu hawa watakula pamoja nami adhuhuri.

Mwanzo 43:17 Genesis 43:17

Yule mtu akafanya kama Yusufu alivyomwambia Naye akawaleta watu hao nyumbani mwa Yusufu.

Mwanzo 43:18 Genesis 43:18

Lakini watu hao wakaogopa kwa sababu wameletwa nyumbani mwa Yusufu, wakasema, Kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humu; apate kutushitaki, na kutuangukia, atutwae sisi kuwa watumwa, na punda zetu.

Mwanzo 43:19 Genesis 43:19

Wakamkaribia yule msimamizi wa nyumba ya Yusufu, wakasema naye mlangoni pa nyumba.

Mwanzo 43:20 Genesis 43:20

Wakamwambia, Tazama, bwana, kweli tulishuka mara ya kwanza ili tununue chakula.

Mwanzo 43:21 Genesis 43:21

Ikawa, tulipofika nyumba ya wageni, tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake, fedha zetu kwa uzani wake kamili; nasi tumezileta tena mikononi mwetu.

Mwanzo 43:22 Genesis 43:22

Nasi tumeleta fedha nyingine mikononi mwetu ili tununue chakula; hatujui ni nani aliyezitia fedha zetu katika magunia yetu.

Mwanzo 43:23 Genesis 43:23

Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia. Kisha akawatolea Simeoni.

Mwanzo 43:24 Genesis 43:24

Mtu yule akawaleta wale watu nyumbani mwa Yusufu, akawapa maji, wakatawadha miguu, akawapa punda zao chakula.

Mwanzo 43:25 Genesis 43:25

Wakaiweka tayari ile zawadi hata atakapokuja Yusufu adhuhuri, maana wamesikia ya kwamba watakula chakula huko.

Mwanzo 43:26 Genesis 43:26

Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka nchi.

Mwanzo 43:27 Genesis 43:27

Akawaulizia hali yao, akasema, Je! Baba yenu, yule mzee mliyemnena, hajambo? Angali hai?

Mwanzo 43:28 Genesis 43:28

Wakasema, Mtumwa wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.

Mwanzo 43:29 Genesis 43:29

Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mamake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu.

Mwanzo 43:30 Genesis 43:30

Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo.

Mwanzo 43:31 Genesis 43:31

Akanawa uso, akatoka, akajizuia, akasema, Leteni chakula.

Mwanzo 43:32 Genesis 43:32

Wakamwandalia yeye peke yake, na wao peke yao, na wale Wamisri waliokula pamoja naye peke yao; maana Wamisri hawawezi kula pamoja na Waebrania, kwa kuwa ni chukizo kwa Wamisri.

Mwanzo 43:33 Genesis 43:33

Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao.

Mwanzo 43:34 Genesis 43:34

Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye.