Mwanzo Mlango 38 Genesis

Mwanzo 38:1 Genesis 38:1

Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.

Mwanzo 38:2 Genesis 38:2

Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.

Mwanzo 38:3 Genesis 38:3

Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.

Mwanzo 38:4 Genesis 38:4

Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.

Mwanzo 38:5 Genesis 38:5

Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.

Mwanzo 38:6 Genesis 38:6

Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.

Mwanzo 38:7 Genesis 38:7

Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; na Bwana akamwua.

Mwanzo 38:8 Genesis 38:8

Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.

Mwanzo 38:9 Genesis 38:9

Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.

Mwanzo 38:10 Genesis 38:10

Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye.

Mwanzo 38:11 Genesis 38:11

Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.

Mwanzo 38:12 Genesis 38:12

Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao manyoya kondoo huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami.

Mwanzo 38:13 Genesis 38:13

Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna, akate manyoya ya kondoo zake.

Mwanzo 38:14 Genesis 38:14

Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe.

Mwanzo 38:15 Genesis 38:15

Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.

Mwanzo 38:16 Genesis 38:16

Akamgeukia kando ya njia, akasema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, Utanipa nini, ukiingia kwangu?

Mwanzo 38:17 Genesis 38:17

Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi wa kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta?

Mwanzo 38:18 Genesis 38:18

Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya muhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.

Mwanzo 38:19 Genesis 38:19

Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake.

Mwanzo 38:20 Genesis 38:20

Yuda akapeleka yule mwana-mbuzi kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami, ili aipate rehani mkononi mwa huyo mwanamke lakini hakumkuta.

Mwanzo 38:21 Genesis 38:21

Akauliza watu wa mahali pale, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba.

Mwanzo 38:22 Genesis 38:22

Akamrudia Yuda akasema, Sikumwona; hata na watu wa mahali hapo walisema, Hakuwako kahaba.

Mwanzo 38:23 Genesis 38:23

Yuda akasema, Na aichukue yeye, tusije tukatiwa aibu; tazama, nimempelekea mbuzi huyu, wala hukumkuta.

Mwanzo 38:24 Genesis 38:24

Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.

Mwanzo 38:25 Genesis 38:25

Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.

Mwanzo 38:26 Genesis 38:26

Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.

Mwanzo 38:27 Genesis 38:27

Ikawa, wakati wake wa kuzaa walikuwapo mapacha tumboni mwake.

Mwanzo 38:28 Genesis 38:28

Ikawa alipokuwa akizaa, mtoto mmoja akatoa mkono, mzalisha akautwaa uzi mwekundu akaufunga mkononi mwake, huku akisema, Huyu ametoka kwanza.

Mwanzo 38:29 Genesis 38:29

Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka. Akasema, Mbona umepita kwa nguvu wewe? Mambo ya nguvu na yakuandame. Kwa hiyo jina lake likaitwa Peresi.

Mwanzo 38:30 Genesis 38:30

Akatoka ndugu yake baadaye, ana uzi mwekundu mkononi mwake; naye akaitwa jina lake Zera.