Mwanzo Mlango 10 Genesis

Mwanzo 10:1 Genesis 10:1

Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.

Mwanzo 10:2 Genesis 10:2

Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.

Mwanzo 10:3 Genesis 10:3

Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.

Mwanzo 10:4 Genesis 10:4

Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.

Mwanzo 10:5 Genesis 10:5

Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.

Mwanzo 10:6 Genesis 10:6

Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.

Mwanzo 10:7 Genesis 10:7

Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.

Mwanzo 10:8 Genesis 10:8

Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.

Mwanzo 10:9 Genesis 10:9

Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.

Mwanzo 10:10 Genesis 10:10

Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.

Mwanzo 10:11 Genesis 10:11

Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;

Mwanzo 10:12 Genesis 10:12

na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.

Mwanzo 10:13 Genesis 10:13

Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,

Mwanzo 10:14 Genesis 10:14

na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:15 Genesis 10:15

Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,

Mwanzo 10:16 Genesis 10:16

na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,

Mwanzo 10:17 Genesis 10:17

na Mhivi, na Mwarki, na Msini,

Mwanzo 10:18 Genesis 10:18

na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.

Mwanzo 10:19 Genesis 10:19

Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.

Mwanzo 10:20 Genesis 10:20

Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.

Mwanzo 10:21 Genesis 10:21

Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana.

Mwanzo 10:22 Genesis 10:22

Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu.

Mwanzo 10:23 Genesis 10:23

Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.

Mwanzo 10:24 Genesis 10:24

Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi.

Mwanzo 10:25 Genesis 10:25

Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.

Mwanzo 10:26 Genesis 10:26

Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera,

Mwanzo 10:27 Genesis 10:27

na Hadoramu, na Uzali, na Dikla,

Mwanzo 10:28 Genesis 10:28

na Obali, na Abimaeli, na Seba,

Mwanzo 10:29 Genesis 10:29

na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani.

Mwanzo 10:30 Genesis 10:30

Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki.

Mwanzo 10:31 Genesis 10:31

Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.

Mwanzo 10:32 Genesis 10:32

Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.