Mwanzo Mlango 25 Genesis

Mwanzo 25:1 Genesis 25:1

Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura.

Mwanzo 25:2 Genesis 25:2

Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua.

Mwanzo 25:3 Genesis 25:3

Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi.

Mwanzo 25:4 Genesis 25:4

Na wana wa Midiani walikuwa, Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote walikuwa ni wana wa Ketura.

Mwanzo 25:5 Genesis 25:5

Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.

Mwanzo 25:6 Genesis 25:6

Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.

Mwanzo 25:7 Genesis 25:7

Hizi ndizo siku za miaka ya maisha ya Ibrahimu alizoishi, miaka mia, na sabini na mitano.

Mwanzo 25:8 Genesis 25:8

Ibrahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.

Mwanzo 25:9 Genesis 25:9

Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni bin Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.

Mwanzo 25:10 Genesis 25:10

Katika lile shamba alilolinunua Ibrahimu kwa wazawa Hethi, huko ndiko alikozikwa Ibrahimu na Sara mkewe.

Mwanzo 25:11 Genesis 25:11

Ikawa, baada ya kufa kwake Ibrahimu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi.

Mwanzo 25:12 Genesis 25:12

Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, ambaye Hajiri, Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Ibrahimu.

Mwanzo 25:13 Genesis 25:13

Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,

Mwanzo 25:14 Genesis 25:14

na Mishma, na Duma, na Masa,

Mwanzo 25:15 Genesis 25:15

na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.

Mwanzo 25:16 Genesis 25:16

Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

Mwanzo 25:17 Genesis 25:17

Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.

Mwanzo 25:18 Genesis 25:18

Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.

Mwanzo 25:19 Genesis 25:19

Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka.

Mwanzo 25:20 Genesis 25:20

Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.

Mwanzo 25:21 Genesis 25:21

Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

Mwanzo 25:22 Genesis 25:22

Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.

Mwanzo 25:23 Genesis 25:23

Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.

Mwanzo 25:24 Genesis 25:24

Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake.

Mwanzo 25:25 Genesis 25:25

Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.

Mwanzo 25:26 Genesis 25:26

Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.

Mwanzo 25:27 Genesis 25:27

Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.

Mwanzo 25:28 Genesis 25:28

Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo.

Mwanzo 25:29 Genesis 25:29

Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana.

Mwanzo 25:30 Genesis 25:30

Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.

Mwanzo 25:31 Genesis 25:31

Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.

Mwanzo 25:32 Genesis 25:32

Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?

Mwanzo 25:33 Genesis 25:33

Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

Mwanzo 25:34 Genesis 25:34

Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.