Mwanzo Mlango 1 Genesis

Mwanzo 1:1 Genesis 1:1

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Mwanzo 1:2 Genesis 1:2

Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Mwanzo 1:3 Genesis 1:3

Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

Mwanzo 1:4 Genesis 1:4

Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.

Mwanzo 1:5 Genesis 1:5

Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Mwanzo 1:6 Genesis 1:6

Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.

Mwanzo 1:7 Genesis 1:7

Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:8 Genesis 1:8

Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mwanzo 1:9 Genesis 1:9

Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:10 Genesis 1:10

Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Mwanzo 1:11 Genesis 1:11

Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:12 Genesis 1:12

Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Mwanzo 1:13 Genesis 1:13

Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Mwanzo 1:14 Genesis 1:14

Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;

Mwanzo 1:15 Genesis 1:15

tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:16 Genesis 1:16

Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.

Mwanzo 1:17 Genesis 1:17

Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi

Mwanzo 1:18 Genesis 1:18

na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Mwanzo 1:19 Genesis 1:19

Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

Mwanzo 1:20 Genesis 1:20

Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.

Mwanzo 1:21 Genesis 1:21

Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Mwanzo 1:22 Genesis 1:22

Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.

Mwanzo 1:23 Genesis 1:23

Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

Mwanzo 1:24 Genesis 1:24

Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:25 Genesis 1:25

Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Mwanzo 1:26 Genesis 1:26

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Mwanzo 1:27 Genesis 1:27

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mwanzo 1:28 Genesis 1:28

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Mwanzo 1:29 Genesis 1:29

Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

Mwanzo 1:30 Genesis 1:30

na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

Mwanzo 1:31 Genesis 1:31

Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.