Mwanzo Mlango 40 Genesis

Mwanzo 40:1 Genesis 40:1

Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri.

Mwanzo 40:2 Genesis 40:2

Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji.

Mwanzo 40:3 Genesis 40:3

Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu.

Mwanzo 40:4 Genesis 40:4

Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumu, nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo.

Mwanzo 40:5 Genesis 40:5

Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani.

Mwanzo 40:6 Genesis 40:6

Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.

Mwanzo 40:7 Genesis 40:7

Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?

Mwanzo 40:8 Genesis 40:8

Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.

Mwanzo 40:9 Genesis 40:9

Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu.

Mwanzo 40:10 Genesis 40:10

Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva.

Mwanzo 40:11 Genesis 40:11

Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.

Mwanzo 40:12 Genesis 40:12

Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu.

Mwanzo 40:13 Genesis 40:13

Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.

Mwanzo 40:14 Genesis 40:14

Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.

Mwanzo 40:15 Genesis 40:15

Kwa sababu hakika naliibiwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda neno lo lote hata wanitie gerezani.

Mwanzo 40:16 Genesis 40:16

Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu.

Mwanzo 40:17 Genesis 40:17

Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.

Mwanzo 40:18 Genesis 40:18

Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu.

Mwanzo 40:19 Genesis 40:19

Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako.

Mwanzo 40:20 Genesis 40:20

Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.

Mwanzo 40:21 Genesis 40:21

Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake.

Mwanzo 40:22 Genesis 40:22

Bali akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyowafasiria.

Mwanzo 40:23 Genesis 40:23

Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau.