Mwanzo Mlango 17 Genesis

Mwanzo 17:1 Genesis 17:1

Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

Mwanzo 17:2 Genesis 17:2

Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.

Mwanzo 17:3 Genesis 17:3

Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,

Mwanzo 17:4 Genesis 17:4

Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,

Mwanzo 17:5 Genesis 17:5

wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.

Mwanzo 17:6 Genesis 17:6

Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.

Mwanzo 17:7 Genesis 17:7

Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.

Mwanzo 17:8 Genesis 17:8

Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.

Mwanzo 17:9 Genesis 17:9

Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.

Mwanzo 17:10 Genesis 17:10

Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

Mwanzo 17:11 Genesis 17:11

Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.

Mwanzo 17:12 Genesis 17:12

Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.

Mwanzo 17:13 Genesis 17:13

Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.

Mwanzo 17:14 Genesis 17:14

Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.

Mwanzo 17:15 Genesis 17:15

Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.

Mwanzo 17:16 Genesis 17:16

Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.

Mwanzo 17:17 Genesis 17:17

Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?

Mwanzo 17:18 Genesis 17:18

Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

Mwanzo 17:19 Genesis 17:19

Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

Mwanzo 17:20 Genesis 17:20

Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.

Mwanzo 17:21 Genesis 17:21

Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.

Mwanzo 17:22 Genesis 17:22

Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu.

Mwanzo 17:23 Genesis 17:23

Ibrahimu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Ibrahimu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.

Mwanzo 17:24 Genesis 17:24

Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake.

Mwanzo 17:25 Genesis 17:25

Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake.

Mwanzo 17:26 Genesis 17:26

Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe.

Mwanzo 17:27 Genesis 17:27

Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na wanunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye.