Mwanzo Mlango 19 Genesis

Mwanzo 19:1 Genesis 19:1

Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.

Mwanzo 19:2 Genesis 19:2

Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.

Mwanzo 19:3 Genesis 19:3

Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.

Mwanzo 19:4 Genesis 19:4

Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.

Mwanzo 19:5 Genesis 19:5

Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.

Mwanzo 19:6 Genesis 19:6

Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.

Mwanzo 19:7 Genesis 19:7

Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.

Mwanzo 19:8 Genesis 19:8

Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.

Mwanzo 19:9 Genesis 19:9

Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.

Mwanzo 19:10 Genesis 19:10

Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.

Mwanzo 19:11 Genesis 19:11

Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.

Mwanzo 19:12 Genesis 19:12

Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;

Mwanzo 19:13 Genesis 19:13

maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu.

Mwanzo 19:14 Genesis 19:14

Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze.

Mwanzo 19:15 Genesis 19:15

Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu.

Mwanzo 19:16 Genesis 19:16

Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.

Mwanzo 19:17 Genesis 19:17

Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.

Mwanzo 19:18 Genesis 19:18

Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu!

Mwanzo 19:19 Genesis 19:19

Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa.

Mwanzo 19:20 Genesis 19:20

Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi.

Mwanzo 19:21 Genesis 19:21

Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena.

Mwanzo 19:22 Genesis 19:22

Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari.

Mwanzo 19:23 Genesis 19:23

Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari.

Mwanzo 19:24 Genesis 19:24

Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana.

Mwanzo 19:25 Genesis 19:25

Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.

Mwanzo 19:26 Genesis 19:26

Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi.

Mwanzo 19:27 Genesis 19:27

Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana,

Mwanzo 19:28 Genesis 19:28

naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru.

Mwanzo 19:29 Genesis 19:29

Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.

Mwanzo 19:30 Genesis 19:30

Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili.

Mwanzo 19:31 Genesis 19:31

Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.

Mwanzo 19:32 Genesis 19:32

Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao.

Mwanzo 19:33 Genesis 19:33

Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.

Mwanzo 19:34 Genesis 19:34

Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye.

Mwanzo 19:35 Genesis 19:35

Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.

Mwanzo 19:36 Genesis 19:36

Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.

Mwanzo 19:37 Genesis 19:37

Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.

Mwanzo 19:38 Genesis 19:38

Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.