Mwanzo Mlango 11 Genesis

Mwanzo 11:1 Genesis 11:1

Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.

Mwanzo 11:2 Genesis 11:2

Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.

Mwanzo 11:3 Genesis 11:3

Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.

Mwanzo 11:4 Genesis 11:4

Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.

Mwanzo 11:5 Genesis 11:5

Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.

Mwanzo 11:6 Genesis 11:6

Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.

Mwanzo 11:7 Genesis 11:7

Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

Mwanzo 11:8 Genesis 11:8

Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.

Mwanzo 11:9 Genesis 11:9

Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.

Mwanzo 11:10 Genesis 11:10

Hivi ndivyo vizazi vya Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika.

Mwanzo 11:11 Genesis 11:11

Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:12 Genesis 11:12

Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela.

Mwanzo 11:13 Genesis 11:13

Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:14 Genesis 11:14

Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.

Mwanzo 11:15 Genesis 11:15

Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:16 Genesis 11:16

Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.

Mwanzo 11:17 Genesis 11:17

Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:18 Genesis 11:18

Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu.

Mwanzo 11:19 Genesis 11:19

Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:20 Genesis 11:20

Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi.

Mwanzo 11:21 Genesis 11:21

Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:22 Genesis 11:22

Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori.

Mwanzo 11:23 Genesis 11:23

Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:24 Genesis 11:24

Nahori akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera.

Mwanzo 11:25 Genesis 11:25

Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na wake.

Mwanzo 11:26 Genesis 11:26

Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani.

Mwanzo 11:27 Genesis 11:27

Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu.

Mwanzo 11:28 Genesis 11:28

Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo.

Mwanzo 11:29 Genesis 11:29

Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.

Mwanzo 11:30 Genesis 11:30

Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.

Mwanzo 11:31 Genesis 11:31

Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.

Mwanzo 11:32 Genesis 11:32

Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.