Mwanzo Mlango 49 Genesis

Mwanzo 49:1 Genesis 49:1

Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.

Mwanzo 49:2 Genesis 49:2

Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.

Mwanzo 49:3 Genesis 49:3

Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.

Mwanzo 49:4 Genesis 49:4

Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.

Mwanzo 49:5 Genesis 49:5

Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri.

Mwanzo 49:6 Genesis 49:6

Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;

Mwanzo 49:7 Genesis 49:7

Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.

Mwanzo 49:8 Genesis 49:8

Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.

Mwanzo 49:9 Genesis 49:9

Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?

Mwanzo 49:10 Genesis 49:10

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.

Mwanzo 49:11 Genesis 49:11

Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.

Mwanzo 49:12 Genesis 49:12

Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

Mwanzo 49:13 Genesis 49:13

Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.

Mwanzo 49:14 Genesis 49:14

Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;

Mwanzo 49:15 Genesis 49:15

Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.

Mwanzo 49:16 Genesis 49:16

Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli;

Mwanzo 49:17 Genesis 49:17

Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali.

Mwanzo 49:18 Genesis 49:18

Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana.

Mwanzo 49:19 Genesis 49:19

Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino.

Mwanzo 49:20 Genesis 49:20

Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme.

Mwanzo 49:21 Genesis 49:21

Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri.

Mwanzo 49:22 Genesis 49:22

Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani.

Mwanzo 49:23 Genesis 49:23

Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi,

Mwanzo 49:24 Genesis 49:24

Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli,

Mwanzo 49:25 Genesis 49:25

Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.

Mwanzo 49:26 Genesis 49:26

Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.

Mwanzo 49:27 Genesis 49:27

Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.

Mwanzo 49:28 Genesis 49:28

Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki.

Mwanzo 49:29 Genesis 49:29

Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;

Mwanzo 49:30 Genesis 49:30

katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

Mwanzo 49:31 Genesis 49:31

Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;

Mwanzo 49:32 Genesis 49:32

shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi.

Mwanzo 49:33 Genesis 49:33

Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.