Mwanzo Mlango 34 Genesis

Mwanzo 34:1 Genesis 34:1

Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi.

Mwanzo 34:2 Genesis 34:2

Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.

Mwanzo 34:3 Genesis 34:3

Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri.

Mwanzo 34:4 Genesis 34:4

Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu.

Mwanzo 34:5 Genesis 34:5

Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja.

Mwanzo 34:6 Genesis 34:6

Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye.

Mwanzo 34:7 Genesis 34:7

Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka.

Mwanzo 34:8 Genesis 34:8

Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe.

Mwanzo 34:9 Genesis 34:9

Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu.

Mwanzo 34:10 Genesis 34:10

Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.

Mwanzo 34:11 Genesis 34:11

Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa.

Mwanzo 34:12 Genesis 34:12

Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu.

Mwanzo 34:13 Genesis 34:13

Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, umbu lao,

Mwanzo 34:14 Genesis 34:14

wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe umbu letu mtu asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu.

Mwanzo 34:15 Genesis 34:15

Lakini kwa sharti hii tu tutapatana nanyi; mkiwa kama sisi, akitahiriwa kila mwanamume wenu,

Mwanzo 34:16 Genesis 34:16

ndipo tutawapa ninyi binti yetu, na sisi tutatwaa binti zenu tutakaa pamoja nanyi, nasi tutakuwa watu wamoja.

Mwanzo 34:17 Genesis 34:17

Lakini kama hamtusikii na kutahiriwa, basi tutamtwaa umbu letu, nasi tutakwenda zetu.

Mwanzo 34:18 Genesis 34:18

Maneno yao yakawa mema machoni pa Hamori, na machoni pa Shekemu, mwana wa Hamori.

Mwanzo 34:19 Genesis 34:19

Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye.

Mwanzo 34:20 Genesis 34:20

Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na watu wa mji wao, wakinena,

Mwanzo 34:21 Genesis 34:21

Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao.

Mwanzo 34:22 Genesis 34:22

Lakini kwa sharti hiyo moja tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila mwanamume, kama hawa walivyotahiriwa.

Mwanzo 34:23 Genesis 34:23

Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu.

Mwanzo 34:24 Genesis 34:24

Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake.

Mwanzo 34:25 Genesis 34:25

Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote.

Mwanzo 34:26 Genesis 34:26

Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka.

Mwanzo 34:27 Genesis 34:27

Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao.

Mwanzo 34:28 Genesis 34:28

Wakachukua kondoo zao, na ng'ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni.

Mwanzo 34:29 Genesis 34:29

Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka.

Mwanzo 34:30 Genesis 34:30

Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.

Mwanzo 34:31 Genesis 34:31

Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee umbu letu kama kahaba?