Mwanzo Mlango 30 Genesis

Mwanzo 30:1 Genesis 30:1

Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.

Mwanzo 30:2 Genesis 30:2

Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?

Mwanzo 30:3 Genesis 30:3

Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye.

Mwanzo 30:4 Genesis 30:4

Basi akampa Bilha mjakazi wake kuwa mkewe. Yakobo akaingia kwake.

Mwanzo 30:5 Genesis 30:5

Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana.

Mwanzo 30:6 Genesis 30:6

Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.

Mwanzo 30:7 Genesis 30:7

Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili.

Mwanzo 30:8 Genesis 30:8

Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.

Mwanzo 30:9 Genesis 30:9

Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.

Mwanzo 30:10 Genesis 30:10

Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.

Mwanzo 30:11 Genesis 30:11

Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.

Mwanzo 30:12 Genesis 30:12

Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.

Mwanzo 30:13 Genesis 30:13

Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri. Akamwita jina lake Asheri.

Mwanzo 30:14 Genesis 30:14

Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.

Mwanzo 30:15 Genesis 30:15

Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang'anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao.

Mwanzo 30:16 Genesis 30:16

Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule.

Mwanzo 30:17 Genesis 30:17

Mungu akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano.

Mwanzo 30:18 Genesis 30:18

Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.

Mwanzo 30:19 Genesis 30:19

Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita.

Mwanzo 30:20 Genesis 30:20

Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.

Mwanzo 30:21 Genesis 30:21

Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina.

Mwanzo 30:22 Genesis 30:22

Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.

Mwanzo 30:23 Genesis 30:23

Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu.

Mwanzo 30:24 Genesis 30:24

Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine.

Mwanzo 30:25 Genesis 30:25

Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.

Mwanzo 30:26 Genesis 30:26

Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia.

Mwanzo 30:27 Genesis 30:27

Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako.

Mwanzo 30:28 Genesis 30:28

Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa.

Mwanzo 30:29 Genesis 30:29

Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu.

Mwanzo 30:30 Genesis 30:30

Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe?

Mwanzo 30:31 Genesis 30:31

Akamwuliza, Nikupe nini? Yakobo akasema, Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda.

Mwanzo 30:32 Genesis 30:32

Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu.

Mwanzo 30:33 Genesis 30:33

Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.

Mwanzo 30:34 Genesis 30:34

Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo.

Mwanzo 30:35 Genesis 30:35

Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe.

Mwanzo 30:36 Genesis 30:36

Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia.

Mwanzo 30:37 Genesis 30:37

Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito.

Mwanzo 30:38 Genesis 30:38

Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa.

Mwanzo 30:39 Genesis 30:39

Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka.

Mwanzo 30:40 Genesis 30:40

Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani.

Mwanzo 30:41 Genesis 30:41

Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito,

Mwanzo 30:42 Genesis 30:42

lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo.

Mwanzo 30:43 Genesis 30:43

Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.