Mwanzo Mlango 50 Genesis

Mwanzo 50:1 Genesis 50:1

Yusufu akamwangukia babaye usoni, akamlilila, akambusu.

Mwanzo 50:2 Genesis 50:2

Yusufu akawaagiza watumishi wake waganga, kwamba wampake baba yake dawa asioze. Waganga wakampaka dawa Israeli.

Mwanzo 50:3 Genesis 50:3

Siku zake arobaini zikaisha, maana hivyo hutimizwa siku za kupaka dawa. Wamisri wakamlilia siku sabini.

Mwanzo 50:4 Genesis 50:4

Siku za kumlilia zilipopita, Yusufu alisema na watu wa nyumba ya Farao, akinena, Kama nimeona neema machoni penu, tafadhalini mkaseme masikioni mwa Farao, mkinena, Baba yangu aliniapisha, akisema,

Mwanzo 50:5 Genesis 50:5

Mimi ni katika kufa, unizike katika kaburi langu nililojichimbia katika nchi ya Kanaani. Basi tafadhali uniruhusu niende sasa nikamzike babangu, nami nitarudi.

Mwanzo 50:6 Genesis 50:6

Farao akasema, Uende, ukamzike baba yako, kama alivyokuapisha.

Mwanzo 50:7 Genesis 50:7

Basi Yusufu akaenda amzike babaye, na watumwa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, wazee wa nyumbani mwake, na wazee wote wa nchi ya Misri.

Mwanzo 50:8 Genesis 50:8

Na nyumba yote ya Yusufu, na nduguze, na nyumba ya babaye; wakawaacha watoto wao tu, na kondoo zao, na ng'ombe zao, katika nchi ya Gosheni.

Mwanzo 50:9 Genesis 50:9

Kisha wakaenda pamoja naye wapanda farasi, na magari; wakawa jeshi kubwa sana.

Mwanzo 50:10 Genesis 50:10

Wakaja mpaka sakafu ya Atadi, iliyo ng'ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya babaye siku saba.

Mwanzo 50:11 Genesis 50:11

Nao waliokaa katika nchi, wale Wakanaani, walipoyaona matanga katika sakafu ya Atadi, wakasema, Matanga haya ya Wamisri ni makuu kwa hiyo mahali pale paliitwa Abel-Misri, iliyo ng'ambo ya Yordani.

Mwanzo 50:12 Genesis 50:12

Wanawe wakamfanyia kama alivyo waagiza;

Mwanzo 50:13 Genesis 50:13

kwa kuwa wanawe wakamchukuwa mpaka nchi ya Kanaani, nao wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia.

Mwanzo 50:14 Genesis 50:14

Yusufu akarudi Misri, yeye na ndugu zake, na wote waliyokwenda pamoja naye kumzika babaye, baada ya kumzika babaye.

Mwanzo 50:15 Genesis 50:15

Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda.

Mwanzo 50:16 Genesis 50:16

Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema,

Mwanzo 50:17 Genesis 50:17

Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.

Mwanzo 50:18 Genesis 50:18

Nduguze wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako.

Mwanzo 50:19 Genesis 50:19

Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu?

Mwanzo 50:20 Genesis 50:20

Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.

Mwanzo 50:21 Genesis 50:21

Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.

Mwanzo 50:22 Genesis 50:22

Akakaa Yusufu katika Misri, yeye na nyumba ya babaye. Akaishi Yusufu miaka mia na kumi.

Mwanzo 50:23 Genesis 50:23

Yusufu akaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu; na wana wa Makiri, mwana wa Manase, walizaliwa magotini mwa Yusufu.

Mwanzo 50:24 Genesis 50:24

Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.

Mwanzo 50:25 Genesis 50:25

Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.

Mwanzo 50:26 Genesis 50:26

Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.