Isaya Mlango 35 Isaiah

Isaya 35:1 Isaiah 35:1

Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.

Isaya 35:2 Isaiah 35:2

Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu.

Isaya 35:3 Isaiah 35:3

Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea.

Isaya 35:4 Isaiah 35:4

Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.

Isaya 35:5 Isaiah 35:5

Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

Isaya 35:6 Isaiah 35:6

Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.

Isaya 35:7 Isaiah 35:7

Na mchanga ung'aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.

Isaya 35:8 Isaiah 35:8

Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.

Isaya 35:9 Isaiah 35:9

Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.

Isaya 35:10 Isaiah 35:10

Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.