Isaya Mlango 25 Isaiah

Isaya 25:1 Isaiah 25:1

Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.

Isaya 25:2 Isaiah 25:2

Kwa sababu umefanya mji kuwa ni chungu; Mji wenye boma kuwa ni magofu; Jumba la wageni kuwa si mji; Hautajengwa tena milele.

Isaya 25:3 Isaiah 25:3

Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza, Mji wa mataifa watishao utakuogopa.

Isaya 25:4 Isaiah 25:4

Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Kivuli wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao, Kama dhoruba ipigayo ukuta.

Isaya 25:5 Isaiah 25:5

Kama vile hari katika mahali pakavu Utaushusha mshindo wa wageni; Kama ilivyo hari kwa kivuli cha wingu, Wimbo wa hao watishao utashushwa.

Isaya 25:6 Isaiah 25:6

Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

Isaya 25:7 Isaiah 25:7

Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote.

Isaya 25:8 Isaiah 25:8

Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo.

Isaya 25:9 Isaiah 25:9

Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.

Isaya 25:10 Isaiah 25:10

Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa.

Isaya 25:11 Isaiah 25:11

Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake.

Isaya 25:12 Isaiah 25:12

Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hata mavumbini.