Isaya Mlango 26 Isaiah

Isaya 26:1 Isaiah 26:1

Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.

Isaya 26:2 Isaiah 26:2

Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

Isaya 26:3 Isaiah 26:3

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

Isaya 26:4 Isaiah 26:4

Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.

Isaya 26:5 Isaiah 26:5

Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, Mji ule ulioinuka, aushusha, Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.

Isaya 26:6 Isaiah 26:6

Mguu utaukanyaga chini, Naam, miguu yao walio maskini, Na hatua zao walio wahitaji.

Isaya 26:7 Isaiah 26:7

Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.

Isaya 26:8 Isaiah 26:8

Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee Bwana; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.

Isaya 26:9 Isaiah 26:9

Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.

Isaya 26:10 Isaiah 26:10

Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa Bwana.

Isaya 26:11 Isaiah 26:11

Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

Isaya 26:12 Isaiah 26:12

Bwana, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.

Isaya 26:13 Isaiah 26:13

Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

Isaya 26:14 Isaiah 26:14

Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.

Isaya 26:15 Isaiah 26:15

Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

Isaya 26:16 Isaiah 26:16

Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

Isaya 26:17 Isaiah 26:17

Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee Bwana.

Isaya 26:18 Isaiah 26:18

Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.

Isaya 26:19 Isaiah 26:19

Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.

Isaya 26:20 Isaiah 26:20

Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.

Isaya 26:21 Isaiah 26:21

Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.