Isaya Mlango 40 Isaiah

Isaya 40:1 Isaiah 40:1

Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.

Isaya 40:2 Isaiah 40:2

Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.

Isaya 40:3 Isaiah 40:3

Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.

Isaya 40:4 Isaiah 40:4

Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa;

Isaya 40:5 Isaiah 40:5

Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.

Isaya 40:6 Isaiah 40:6

Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni;

Isaya 40:7 Isaiah 40:7

Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani.

Isaya 40:8 Isaiah 40:8

Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

Isaya 40:9 Isaiah 40:9

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.

Isaya 40:10 Isaiah 40:10

Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.

Isaya 40:11 Isaiah 40:11

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Isaya 40:12 Isaiah 40:12

Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?

Isaya 40:13 Isaiah 40:13

Ni nani aliyemwongoza roho ya Bwana, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake?

Isaya 40:14 Isaiah 40:14

Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya fahamu?

Isaya 40:15 Isaiah 40:15

Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.

Isaya 40:16 Isaiah 40:16

Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara.

Isaya 40:17 Isaiah 40:17

Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni ya si kitu, na ubatili.

Isaya 40:18 Isaiah 40:18

Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?

Isaya 40:19 Isaiah 40:19

Sanamu fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha.

Isaya 40:20 Isaiah 40:20

Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.

Isaya 40:21 Isaiah 40:21

Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia?

Isaya 40:22 Isaiah 40:22

Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;

Isaya 40:23 Isaiah 40:23

ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia.

Isaya 40:24 Isaiah 40:24

Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.

Isaya 40:25 Isaiah 40:25

Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu.

Isaya 40:26 Isaiah 40:26

Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.

Isaya 40:27 Isaiah 40:27

Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?

Isaya 40:28 Isaiah 40:28

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Isaya 40:29 Isaiah 40:29

Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

Isaya 40:30 Isaiah 40:30

Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

Isaya 40:31 Isaiah 40:31

bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.