Isaya Mlango 63 Isaiah

Isaya 63:1 Isaiah 63:1

Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?

Isaya 63:2 Isaiah 63:2

Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?

Isaya 63:3 Isaiah 63:3

Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.

Isaya 63:4 Isaiah 63:4

Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.

Isaya 63:5 Isaiah 63:5

Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.

Isaya 63:6 Isaiah 63:6

Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini.

Isaya 63:7 Isaiah 63:7

Nitautaja wema wa Bwana, sifa za Bwana kwa yote aliyotukirimia Bwana; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.

Isaya 63:8 Isaiah 63:8

Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao.

Isaya 63:9 Isaiah 63:9

Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.

Isaya 63:10 Isaiah 63:10

Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.

Isaya 63:11 Isaiah 63:11

Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu?

Isaya 63:12 Isaiah 63:12

Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kuume wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele?

Isaya 63:13 Isaiah 63:13

Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae?

Isaya 63:14 Isaiah 63:14

Kama ng'ombe washukao bondeni, Roho ya Bwana akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.

Isaya 63:15 Isaiah 63:15

Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.

Isaya 63:16 Isaiah 63:16

Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.

Isaya 63:17 Isaiah 63:17

Ee Bwana, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.

Isaya 63:18 Isaiah 63:18

Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.

Isaya 63:19 Isaiah 63:19

Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.