Isaya Mlango 46 Isaiah

Isaya 46:1 Isaiah 46:1

Beli anaanguka chini, Nebo anainama; sanamu zao ziko juu ya wanyama, na juu ya ng'ombe; vitu vile mlivyokuwa mkivichukua huku na huku vimekuwa mzigo, mzigo wa kumlemea mnyama aliyechoka.

Isaya 46:2 Isaiah 46:2

Wanajiinamisha, wanainama pamoja; hawakuweza kuutua mzigo, bali wao wenyewe wamekwenda kufungwa.

Isaya 46:3 Isaiah 46:3

Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;

Isaya 46:4 Isaiah 46:4

na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.

Isaya 46:5 Isaiah 46:5

Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa?

Isaya 46:6 Isaiah 46:6

Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu.

Isaya 46:7 Isaiah 46:7

Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa na taabu yake.

Isaya 46:8 Isaiah 46:8

Kumbukeni haya, mkajionyeshe kuwa waume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao;

Isaya 46:9 Isaiah 46:9

kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;

Isaya 46:10 Isaiah 46:10

nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.

Isaya 46:11 Isaiah 46:11

Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.

Isaya 46:12 Isaiah 46:12

Nisikilizeni, ninyi mlio na moyo mshupavu, mlio mbali na haki;

Isaya 46:13 Isaiah 46:13

Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.